ASKARI polisi watatu Mkoani Iringa, wamejeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao wakati wakimkamata mtuhumiwa sugu wa makosa ya wizi wa pikipiki na uvunjaji, Godson Kahemela.
kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi` alisema askari hao walijehuriwa wakati wakimthibiti mtuhumiwa huyo ambaye amekuwa akijihusisha na matukio ya uvunjaji katika maeneo mbalimbali manispaa ya iringa. mwandishi Francis Godwin anaripoti .
Kamanda Bukumbi alisema ''Mtuhumiwa huyu wakati anakamatwa aliwajeruhi askari watatu sehemu mbalimbali na alipokamatwa alikutwa na panga aliloliandika KIFO, akimaanisha kuwa yuko tayari kufanya mauaji kama ambavyo alitaka kuwafanyia askari wakati anakamatwa,'' alisema kamanda Bukumbi.
Wakati huo huo, Kamanda Bukumbi Jeshi la polisi kwa kushirikiana na maofisa uhamiaji wa mkoa wa Iringa wamewakamata wahamiaji 40, raia wa Ethiopia, ambao wanadaiwa ya kuingia nchini kinyume cha utaratibu.
Alisema wahamiaji hao walikamatwa wilaya Iringa katika Barabara kuu ya Iringa -Mbeya baada ya kutelekezwa katika lori aina ya Mitsubishi Fuso lenye namba za usajili T 517 DJY mali ya Deogratius Kimambo, mkazi wa mkoani Kirimanjaro.
Kamanda Bukumbi amesema kukamatwa kwa wahamiaji hao ni muendelezo wa operesheni mbalimbali zinazoendelea mkoani Iringa zenye lengo ya kupambambana na matukio ya uhalifu.
Alisema baada ya kufanya upekuzi katika gari hilo walikutwa wahamiaji ha wakiwa wameingia nchini kupitia mpaka wa Namanga, wakisafirishwa kwenda mpaka wa Tunduma.
Pia alisema Januari 11, mwaka huu polisi kwa kushirikiana na maofisa wa hifadhi ya Taifa Ruaha, waliwakamata watu wawili wakisafirisha meno ya tembo vipande 19 pamoja na jino moja la kiboko kwa kutumia pikipiki
Kamanda Bukumbi aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Ezekiel Patrick (43) na George Ng'umbi (25). Kadhalika, alisema januari 7, mwaka huu, maeneo ya kitongoji cha Magunga Bondeni, Kiponzero Wilayani Iringa, askari polisi walimkamata Paul Kalinga (47) akiwa na meno mawili ya tembo
0 Comments