Mwanafuzi wa shahada ya uhasibu wa chuo cha uhasibu Arusha,IAA,Juma Masende aweka nia ya kuwania nafasi ya spika wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania.................Teddy Kilanga_Arusha
Akizungumza chuoni hapo,Masende alisema lazima achukue fomu ya kuwania nafasi hiyo ili aweze kusaidia serikali katika kusimamia rasilimali za nchi pamoja na matumizi bora ya rasilimali.
"Tutawakaribisha wawekezaji nchini na watafuta misingi tuliojiwekea na mimi nitakwenda kusimamia kanuni na sheria za nchi kikamilifu kwani ndio mwongozo wetu,"alisema Masende.
Alisema atasimimia kanuni ili kila Mtanzani aweze kunufaika na rasilimali za nchi pasipokuwepo upendeleo wowote kwani kiongozi anatakiwa kuwa muwazi namzalendo ambapo wanategemea kupambania rasilimali ziliopo nchini kwa maslahi ya nchi.
"Tuna uhakika kuwa nchi yetu hii ni tajiri sana kwasababu tunarasilimali nyingi ambazo tukizisimamia kupitia kanuni zetu kwa mwenendo mzuri pasipokuvunja sheria kila Mtanzania mmoja mmoja atanufaika,"alisema.
Masende alisema vijana ndio nguzo ya Taifa wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii wakimuunga mkono Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
0 Comments