Header Ads Widget

MNF YATAMBULISHA WAJUMBE WA BODI WAPYA

 




Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam 


Taasisi ya  Mwalimu Nyerere (MNF) leo imewatambulisha wajumbe wapya nane wa bodi ya Taasisi hiyo, ambao wanafanya kuwa na idadi ya wajumbe 10, huku ikimteua Joseph Butiku kuwa Mwenyekiti wa Taasisi.


Aidha, wajumbe hao, ni pamoja na Balozi Amina Salum Ali,Neema Nyerere Drago,Geofrey Israel Kirenga, Kathryn Ngenda Kigaraba, John Joel Kyaruzi, Balozi Celestine Christopher Liundi, Prof Penina Oniviel Mlama, Profesa Martha Ambrose Suley Qorro, huku wajumbe wa zamani akiwa ni Joseph Butiku na ProfTarsis Bazana Kabwegyere.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mara baada ya kutambulisha wajumbe hao, Mwenyekiti  mpya wa MNF Joseph Butiku amesema kuwa, tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo miaka 26 iliyopita, Taasisi hiyo imekua ikisimamia Serikali katika masuala ya Amani,Umoja na Maendeleo ya Watu.


Aidha amesema kwamba  Malimu Julius Kambarage Nyerere alianzisha Taasisi hiyo mara baada ya kustaafu uongozi ikiwa lengo ni kusimamia misingi ya Utu,Umoja na Kudumisha Amani pamoja nakuhimiza wananchi katika kujiletea maendeleo.



Amesema Taasisi hiyo licha yakukumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa fedha za kujiendesha,  imekua na heshima kubwa kwa Taifa nakwambia uongozi uliopo utaendelea kusimamia misingi iliyoasisiwa na baba wa Taifa pindi akianzisha Taasisi hiyo kwa ajili yukuwaletea maendeleo Watanzania.


" Taasisi yetu tumekua tukijikita kuwafikia wananchi nakuwahimiza wawe na Umoja na mshikamano,pasipo na Umoja hakuna maendeleo,hivyo tunawaelimisha wawe na Umoja na kufanya kazi za kuwaletea maendeleo" amesema Butiku.


Kwa upande wake,  aliekua Kaimu Mwenyekiti wa Taasisi hiyo,Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba amesema kuwa, tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo imepata mafanikio mbalimbali ikiwemo kupata jengo linalotumika kama kitega uchumi na ofisi ambacho kinawapatia fedha kwa ajili kujiendesha japo sio kwa kiwango kikubwa.



"Tulianza kutafuta kitega uchumi na tukapata kiwanja Mtaa wa Sokoinne karibu na ukumbi wa Karemjee,lakini wakati tulipotaka kuanza ujenzi Serikali ikasema hairuhusiwi kujenga jengo la zaidi ya ghorofa sita karibu na Ikulu hivyo ikatupatia kiwanja kingine Mtaa wa jiji ndo tumejenga jengo letu " amesema Jaji Warioba 


Aidha, amesema licha yakua na jengo hilo lakini  bado hawajapata fedha za kutosha, hivyo, wanaiomba Serikali na wadau mbalimbali wawezeshe kupata fedha, kutokana na kukosa wapangaji wa uhakika tangu Serikali ilipohamia Dodoma pamoja na kutokea  mripuko wa ugonjwa wa UVIKO 19 miezi michache baada ya jengo hilo kufunguliwa.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI