Teddy Kilanga _Arusha
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha ( Arusha DC) ametoa pongezi kwa wana Arumeru kwa jinsi wanavyoungana kila mwaka na kujadili maswala ya maendeleo katika Jimbo na katika Halmashauri yao.
Mwenyekiti huyo Mh Ojung'u Salekwa ameyasema hayo alipokuwa akiongea na umoja wa wana Arumeru (AM) waliokutana katika mpango wao uitwao Get Together iliyoandaliwa na wana Arumeru hao uliolenga kuwakutanisha wana ARUMERU.
Aidha katika mkutano huo wana Arumeru walitoa kero mbalimbali kama Elimu, Umeme, miundombinu huku wakipongeza pia kazi inayofanyika katika Arumeru Magharibi.
Katika kujibu kero hizo Mwenyekiti wa Halmshauri Mh Salekwa ambaye ni diwani wa kata ya Laroi Mkoani Arusha amesema kuwa, serikali imejipanga kwa mwaka 2022 katika kukamilisha maswala haya ya maendeleo katika kata zote katika Jimbo hili la Arumeru Magharibi.
Mh. Salekwa ametoa rai pia kwa makundi mbalimbali katika kata kama ya vijana, wanawake na wenye Ulemavu kuchangamkia fursa ya asilimia zinazotolewa na serikali katika majimbo yote na wilaya zote nchini kama mikopo.
Aidha amewaasa madiwani wa viti maalum kuelezea maswala ya maendeleo katika maeneo yao huku akiwaasa wana Arumeru Magharibi (AM) Kuanzia katika kata zao wakiwa wameungana katika vikundi kwa mujibu wa sheria.
Naye Mwenyekiti wa Kikao Mh. Bon Tarakwa aliyekuwa Diwani Mstaafu wa Mwandeti aliwapongeza wana AM kwa kuaanda dhifa hii huku akiomba wana AM kufanya vikao kama hivi kila mwaka ili kufanya tathmini ya maswala ya maendeleo katika jimbo lao.
Arumeru Magharibi (AM) inawakumbusha wananchi wote waliopo katika Jimbo la Arumeru Magharibi na nje ya Mkoa wa Arusha.
Jumla ya wana AM waliokutana ni watu wapatao 34 wakiwepo viongozi wanaounda kata kama Madiwani na madiwani wa viti maalum na uwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi Mh Noa Ole Saputu.
0 Comments