Kiongozi wa kanisa la Uponyanji nchini Nabi Joshua amewataka baadhi ya watu Wanaomkatisha Tamaa Rais Samia Suluhu Hassan kuacha Mara moja kwani hata biblia imelekeza kuhusu Mikopo.
Nabiii Joshua ameyasema hayo wakati wa ibada maalumu iliyofanyika katika kanisa Hilo Lililopo Kihonda Yespa Mjini Morogoro ambapo amesema biblia imesema kukopa sio dhambi ila dhambi ni kutorudisha hivyo Rais Samia yupo sahihi katika Suala Hilo.
Hivi karibuni zimeibuka baadhi ya hoja kwenye mitandao zikisema kuwa endapo Rais Samia ataendeleo kukopa ipo siku nchi itauzwa Jambo ambalo limezua taharuki kwa wananchi.
Katika hatua nyingine Nabii Joshua amempongeza Rais Kwa kuendelea kutekeleza miradi ya kimkakati iliyoanzishwa na Serikali ya awamu ya tano
Joshua anasema miradi mikubwa Kama Ujenzi wa bwawa la Mwalimu Nyerere,reli ya kisasa inaendelea vizuri Jambo ambalo linaleta Faraja kwa Watanzania.
"wapo watu wengi walikua na wasiwasi kuhusu utendaji kazi wa Rais Samia lakin kwa Sasa kila mmoja ameamkubali namna anavyopambana kutekeleza miradi hivyo kila mmoja anapaswa kumpongeza na KUmuunga mkono"Nabii Joshua .





0 Comments