Header Ads Widget

WAZIRI DKT. NDUMBARO AWATAKA WAKAZI WA JIMBO LA SONGEA MJINI KUITANGAZA HIFADHI YA RUHILA .

 

   





WAZIRI wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea mjini Mkoani Ruvuma Dkt Damas Ndumbaro amewataka wakazi wa Jimbo hilo na maeneo mengine kuitumia Hifadhi ya Wanyamapori ya Ruhila(ZOO) kwa kufanyia shughuli za mikutano au sherehe ili kuitangaza hifadhi hiyo katika maeneo mbalimbali......NA AMON MTEGA, _SONGEA.



Dkt Ndumbaro ametoa wito huo wakati akizungumza na mamia  ya  wakazi wa jimbo hilo ambao walihudhuria sherehe za mwaka mpya wa 2022 katika eneo la hifadhi hiyo ambayo inasimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA)ipo ndani ya Manispaa ya Songea mkoani humo .




Waziri Dkt Ndumbaro akizungumza na wakazi hao ambao katika sherehe hiyo walipata kitoweo cha nyama pori (Nyati) amesema kuwa wakazi wa Jimbo hilo wanakila sababu ya kujivunia hifadhi hiyo kwa kuwa ipo mjini Songea  jambo ambalo hata utalii wake hautumii garama kubwa kufika katika eneo la hifadhi hiyo .




 Licha ya kuwataka wakazi hao kuitangaza hifadhi hiyo kwa kwa kwenda kufanyia vikao mbalimbali pamoja na sherehe amesema kuwa Wizara imejipanga kupaboresha zaidi kwa kujenga uzio ambao umeshatengewa fedha Sh.Milioni mia tano (sh.500 milioni) ambazo zimetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kuboresha sekta ya utalii ili kuwavutia watalii wengi hapa Nchini.





 Dkt Ndumbaro ambaye hadi sasa akiwa jimbo kwake ameshatembelea milima ya uhifadhi wa Misitu ya Matogoro kisha kuzungumza na mamia ya wakazi wa Jimbo hilo amesema kuwa katika mikakati ya kuboresha hifadhi hiyo ni pamoja na kuongeza Wanyama ambao wanadaiwa ni wakali kama Simba ,Chuwi ,Mamba na Twiga ili watalii wakifika katika eneo hilo wasikose kuwaona wanyama hao na kuwa ameshapatikana mwekezaji atakayejenga hoteli katika eneo hilo kwaajili ya wageni wa kutoka mikoa mbalimbali.



Aidha Waziri huyo akiwa katika hifadhi hiyo alipita kuizungukia baadhi ya maeneo ambayo yemetegwa kwaajili ya uwekezaji wa vitu mbalimbali ambapo katika mizunguko hiyo ametumia usafiri  wa Baiskeli .





 Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Songea mjini Hamis Abdalah Ally amewapongeza wafanyakazi wa TAWA,kwa kazi kubwa wanayoifanya katika hifadhi hiyo hasa ya kuilinda miti ya asili (Pori)isivamiwe na watu ambao hawajui nini maana ya uhifadhi .




Naye mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho amempongeza Waziri Dkt Damas Ndumbaro kwa kutekeleza ilani ya CCM kikamilifu katika sekta ya Maliasili na Utalii jambo ambalo limefanya kuwaleta watalii wengi kwenye vivutio mbalimbali vya hapa Nchini.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI