Header Ads Widget

CCM KILIMANJARO YAMTAKA SPIKA NDUGAI KUTOKA HADHARANI NA KUOMBA MSAMAHA KWA RAIS SAMIA NA WATANZANI KUTOKANA NA KAULI YAKE YA FEDHEA ALIYOITOA.



NA WILLIUM PAUL, MOSHI.


CHAMA cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro kimelaani kauli ya fedhea iliyotolewa na Spika wa Bunge la Muungano wa Tanzania Job Ndugai kuwa nchi hii itapigwa mnada na kumtaka kutoka hadharani na kuomba msamaha kwa Rais Samia Suluhu Hasani na Watanzania kutokana na kauli hiyo.



Chama hicho kimesema kuwa kauli hiyo ni ya uchochezi kwani kabla kuchukuliwa kwa mkopo wa trilioni 1.3 kamati ya fedha ya Bunge ilishirikishwa na kukaa na kujadili matumizi yake.



Tamko hilo lilitolewa jana na Mwenyekiti wa ccm mkoa, Patrick Boisafi alipozungumza na wanahabari ambapo alisema kuwa, mwanachama huyo wa CCM, mjumbe wa kamati kuu na msimamizi wa muimili wa nchi ametoa kauli ya kufedhehesha kwa Rais.




"Kauli ya trilioni 1.3 fedha za mkopo zinaweza kupelekea nchi kupigwa mnada ni fedhea na ni kauli ya uchochezi kwani huyo aliyeitoa mwenyewe alishirikishwa mwanzo kabla ya mkopo haujachukuliwa na kuunga mkono iweje leo anatoka hadharani na kutoa lugha za fedhea kwa Rais na watanzania" alisema Boisafi.


Alisema kuwa, Rais aliona kunahitaji wa madarasa 15000 ambapo kama hayatapatikana Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu hawatapa pa kusomea  pamoja na uhitaji wa vituo vya afya.


Boisafi aliendelea kudai kuwa, Rais alikutana na  wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa, wakuu wa mikoa na makatibu tawala mikoa na kutoa mwelekeo na kuomba fedha hizo zisimamiwe vizuri na kazi ionekane na ndicho kilichofanyika kupitia mkopo huo.


"Kama fedha hizo trilioni 1.3 zisingekuwepo hali ingekuwa mbaya katika sekta ya elimu ambayo ingepelekea wananchi kuchangishwa fedha za ujenzi wa madarasa lakini kwa kipindi hiki hili halipo" alisema Boisafi.

Mwenyekiti huyo alidai kuwa, kitendo cha Ndugai kutoa kauli hiyo ya fedhea ni kulewa madaraka na kumtaka ajitafakari kwani yeye amekuwa kwenye sistimu kipindi cha nyuma na ameshuhudia nchi ikikopa lakini haijawahi kupigwa mnada.


Aidha alitumia nafasi hiyo kuwaomba Watanzania kuwa wazalendo na waungwana kuipenda nchi na kuunga mkono kazi zinazofanywa na Rais Samia.

Kwa upande wake, Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa kupitia mkoa wa Kilimanjaro (MNEC), Selemani Mfinanga alisema kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia imekuwa ya wazi na ya ushirikishaji wananchi kwa kila jambo na amejitoa kuhakikisha maendeleo yanafika kila mkoa.



Mfinanga alisema kuwa, hata uchukuaji wa mkopo wa trilioni 1.3 aliwashirikisha viongozi mbalimbali wa serikali na chama hivyo kitendo cha baadhi ya watu kutoa kauli za kumkebei Rais haziwapendezi Watanzania na kuwataka kujitafakari.

Mwisho...

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI