Na Mwandishi Wetu, Chalinze.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwani Kikwete ameendelea na ziara yake maalumu ikiwemo kutatua migogoro ya ardhi, sambamba na kukagua shule zinazojengwa kwa fedha za maendeleo.
Mh. Ridhiwan Kikwete emeweza kutembelea katika Vijiji vya Mindutulieni, Kinzagu na Lugoba ambapo kote huko ameweza kufanya mikutano ya wazi kusikia na kupokea kero na maoni ya wananchi.
Akiwa katika ziara hiyo, Mh. Ridhiwan Kikwete alibainisha kuwa ofisi yake na yeye kama Mbunge watahakikisha wanafika kwa Wananchi mara kwa mara ilikusikiliza na kutatua kero zao zinazowakabiri huku zile zingine akizIpokea na kuziwasilisha ngazi za juu ikiwemo Bungeni na Serikalini.
"Hatua zinazochukuliwa kutatua migogoro ya ardhi inayosababisha na watu wasiofuata taratibu ndiyo zinazitaraji kuwa chachu ya kurudisha amani na maendeleo katika miji yetu…”Alibainisha Mh. Ridhiwani Kikwete
Aidha, aliendelea kutoa shukrani kwa Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutoa fedha zilizosaidia na zinazoendelea kusaidia miradi mbalimbali ndani ya Halmashauri na Jimbo hilo la Chalinze ikiwemo Bilioni 1.7 katika ujenzi wa Madarasa, mabweni na huduma za afya ikiwemo ujenzi wa Hospitali.
"Chalinze kazi zinaendelea, Wanachalinze kila kona wanafurahia matunda mema ya Serikali chini ya Rais wetu Mh. Samia Suluhu Hassan." Alimalizia Mh. Ridhiwan Kikwete.
0 Comments