Header Ads Widget

JESHI LA WANAMAJI WA PAKISTANI WAHUDUMIA WATU 2000 KWENYE KAMBI YA MATIBABU DAR




Na Andrew Chale, Dar es Salaam.



JESHI la Wanamaji maji la Pakistan wanaotembea nchi mbalimbali duniani kote kwa kutumia meli ya kubwa ya matibabu (Navy Ship ) au "PNS ALAMGIR" kwa kushirikiana na Ubalozi wa Nchini hiyo hapa Tanzania, umeendesha huduma za kibingwa za matibabu pamoja na utoaji wa dawa bure kwa watu zaidi ya 2000.


Huduma hiyo ya matibabu bure ya siku mbili yameendeshwa katika ukumbi mkubwa wa Diamond Jubilee- Agha Khan uliopo Upanga, Dar es Salaam.



Awali Ubalozi wa Pakistan ulieleza kuwa, matibabu hayo ya bure ni kwa watu wote wa Tanzania na Wana Diaspora wa Pakistan wanaoishi Tanzania.


Kwa mujibu wa mmoja wa jumuiya za kutoa huduma katika kambi hiyo Bw. Riaz Ahemed kutoka Jumuiya ya Memon Jamaat alisema kuwa siku ya kwanza waliweza kuhudumia watu zaidi ya 400 na watu zaidi 1600 siku ya mwisho.


"Kambi hii ya matibabu tumeendelea kutoa huduma ambapo jana January 11 watu. Zaidi ya 400 wamepatiwa huduma.



Lakini leo hadi kufika saa sita mchana tumeshahudumia watu zaidi ya 1500 na wengine bado wapo nje wanaendelea kujiandikisha." Alisema Riaz. 


Baadhi ya Huduma hizo ni pamoja na tiba ya memo, magonjwanwa moyo, kisukari, presha huku wakitoa ushahuri wa kitalaam kutoka kwa Madaktari bingwa sambamba na kupatiwa dawa bure.



Jumuiya zilizotoa ushirikiano wa kuendeleza kambi hiyo ni pamoja na Memon Jamaat, Kokni Muslim Jamaat, Sunni Muslim Jamaat.


Hii ni mara kwanza kutoa huduma hizo za  matibabu hapa nchini ambapo meli hiyo ya madaktari wa Kijeshi wa kwenye maji inatarajiwa kuelekea nchini Kenya kuendesha kambi kama hiyo.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI