Askofu wa kanisa katoriki wa jimbo la Same,Rugath Kimaro amesema kanisa lina juhudi katika harakati za kuiwezesha jamii kwa kutumia maarifa na ujuzi katika kuleta maendeleo ya kweli.Mwandishi wa Matukio Daima Teddy Kilanga anaripoti toka Arusha
Akizungumza katika chuo cha mtakatifu Agustine,Askofu Kimaro amesema lengo la chuo hicho kinalengo kuwa kituo bora cha elimu,utafiti pamoja na utumishi wa umma pamoja na kukuza harakati na ulinzi wa kweli ulio katika uwazi na uaminifu na umahiri katika utoaji wa huduma
Askofu Rugath alisema pamoja na hayo pia chuo hicho kimelenga kutunza mali binafsi na umma katika kuhamasisha maendeleo ya jumla katika utoaji wa elimu bora kwa uchambuzi na dhamira kwa kutoa huduma kwa ukarimu pamoja na heshima kwani ni tunu za masingi ambazo kama Taifa tunajivuania.
"Kanisa linatambua wazi kuwa ili kuwa na jamii yenye maendeleo ya kweli tunahitaji kufanya kazi kwa ushirikiano kwani tusipofanya hivyo twaweza kujenga matabaka yawaliyonacho na wasionacho,"amesema Askofu huyo.
Amesema wanapaswa kutumia rasilimali zilizopo ili kuiwezesha jamii katika kuleta maendeleo ya kweli kama waliofanya watu mashuhuri duniani hivyo mabadiliko ya tabia ya nchi yanaleta madhara kwa jamii pamoja na kizazi kijacho.
Naye Mkurugenzi wa tawi la Arusha,Dkt.Charles Rufiriza amesema ni vyema jitihada za serikali zikazidi kubimarishwa ili watu wengi wapate kunufaika.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Mhandisi Richard Ruyango amesema anashukuru mamlaka za taasisi za dini kwa kazi za utoaji wa elimu kwa watanzania kupitia taasisi zao za dini katika kutengeneza rasilimali za watu kwa kuleta maendeleo nchini.
0 Comments