Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Aliyekuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ambaye kwa sasa ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum mapema leo amemkabidhi Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu Wizara hiyo.
Waziri Ummy Mwalimu kabla ya Uteuzi wa sasa alikuwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais -TAMISEMI.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Wizara zilizoko katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma ambapo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Waziri Dkt. Godwin Mollel, Katibu Mkuu Prof. Abel Makubi, Naibu Katibu Mkuu Dkt. Seif Shekalaghe.
Wengine walioshuhudia tukio hilo ni Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichalwe pamoja na Wakurugenzi na Menejimenti ya Wizara ya afya.
0 Comments