Taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza inasema kuwa Ibada Maalumu ya kuwaaga Marehemu wa ajali ya Maafisa Habari na Waandishi waliofariki leo itafanyika kesho kuanzia saa 2:00 asubuhi katika Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Baada ya Ibada taratibu zitakazofuata zitakuwa kama ifuatavyo;
1. Mazishi ya Mwili wa Husna Mlanzi yatafanyika kesho saa 10 jioni jijini Mwanza.
2. Mwili wa Antony Chuwa utasafirishwa kwa gari kwenda Moshi.
3. Mwili wa Johari utasafirishwa kwa gari kwenda Arusha.
4. Mwili wa Abel Ngapemba utasafirishwa kwa ndege kwenda Dar es Salaam; na
5. Mwili wa Steven Msengi utasafirishwa kwenda Dar es Salaam kwa gari.
Taarifa zingine zitatolewa baadae kadri tutakavyozipokea.
Tuzidi kuwaombea wenzetu.
Katibu Mkuu
TAGCO
11/01/2022
0 Comments