Header Ads Widget

ASILIMIA 10 KATI YA 86 YA MIRADI INAYOBUNIWA NA VIJANA NDIO INAYODUMU

IMEELEZWA  kuwa     kati ya  asilimia 86 ya  mawazo ya  miradi ya  kimaendeleo inayoibuliwa na  vijana  nchini Tanzania ni asilimia 10  pekee ya  mawazo  hayo  ndio  ambayo yamekuwa  yakitekelezwa na kuleta mafanikio kwa  walioibua mawazo hayo .    


Kuwa   sehemu  kubwa  ya  mawazo yanayoibuliwa   yamekuwa  hayana mafanikio  kutokana na   wahusika  kuibua  kuibuka na mawazo ya  miradi  wasiyoweza  kuisimamia  zaidi ya kuibua  kwa  hisia  za  tamaa toka kwa  wengine.

Akitoa  mafunzo ya  ujasiliamali  Leo   katika  Ukumbi  wa Fox  Igoda  Mufindi ,Mwezeshaji  wa mafunzo ya  kuwajengea  uwezo vijana  waliopo katika mradi  wa  Youth  Agency Mufindi(YAM) John Kalolo  alisema  kuwa  tamaa ya  baadhi ya  waibuaji  wa  miradi ya  kimaendeleo  imekuwa  ikipelekea  miradi  hiyo  kutofanikiwa kutokana na kutokuwa na malengo  sahihi ya  uendeshaji  wa  miradi  hiyo .

Hivyo  alisema lazima  vijana  ambao  wanahitaji  kufanikiwa katika  uibuaji  wa  miradi  na  uandishi wa  miradi ni lazima  kwanza  kuwa  ari ya  kuisimamia na  kuifanya  miradi  husika  kwa  kutanguliza  kipaji  cha  uendeshaji  wa  miradi  husika  na  sio  kufanya kwa  kuiga kwa  wengine.


" Kwenye  maisha  wengi  waliofanikiwa ni  wale  ambao  wanafanya shughuli  ambazo  wanazipenda  kutoka  moyoni na  sio  wale  ambao  wanafanya  miradi ya  kuiga  kutoka kwa  wengine ama  kwenda  kuandika andiko la  mradi ambao  huna  uwezo nao  kuufanya amini utashindwa  kufika  mbali katika mradi  wako "  alisema

Serikali na  wadau  mbali mbali wamekuwa  wakitenga  fedha  kwa  ajili ya  kuwezesha  vijana  na kati ya  fedha   hizo ni pamoja na  fedha  zinazotolewa na Halmashauri  za  wilaya  nchini  kupitia makusanyo  yake ya ndani  ambapo  vijana  wametengewa asilimia 4  kati ya  asilimia 10  zinazotolewa na Halmashauri  nchini.

Hivyo  iwapo   vijana   watakimbilia  kuandika miradi ama  kuanzisha  vikundi  bora  mradi  wapate   fedha  hizo  ndio  mwanzo  wa  vikundi ama  miradi  husika   kufa kabla ya  kufika  mbali.   

Pia  alisema    baadhi ya  vijana  wameshindwa  kufanikiwa  katika maisha  kutokana na  kutanguliza  imani potofu  hata  baadhi yao  kutegemea  nguvu  za  giza na kujikuta  wanaingia katika mikono ya  sheria  kwa  kudanganywa na  waganga   kwenda  kufanya vitendo  vya  mauwaji ama  vitendo   viovu kwenye jamii  ili  kupata  utajiri wa  haraka  haraka.

Zilipa Mgeni  ni  meneja  mradi  wa YAM alisema lengo la mafunzo hayo yamelenga  kuwawezesha  vijana  zaidi ya  770 wakiwemo  watoto  150  kutoka   kata  tatu  za  Ihanu , Igoda na  Luhunga  kama  ambazo  zote  zitaunganishwa na  vijiji  16  za  mradi  huo .

Washiriki  wa mafunzo hayo  Kelvin  Mnyamka  na  Zelida Deule    mbali  ya  kupongeza mradi  huo wa YAM kwa  kuwaunganisha katika mradi  huo  bado   walisema mfunzo hayo ni  fursa  kubwa kwao  kusonga  mbele katika shughuli za  kiujasiliamali  kwani awali  walikuwa  nyuma kutokana na  kutawaliwa na mawazo  potofu .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI