SERIKALI imeziagiza Mamlaka zote zinahusika na Utoaji wa huduma za Afya nchini kuwachukulia hatua za kisheria watumishi wa Afya watakaobainika kuwanyanyapaa na kuwabagua watu wanaoishi na Virusi vya ukimwi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema hayo leo wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Mbeya.
Aidha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mafanikio ya Serikali katika kupambana na maambukizi ya Virusi ya UKIMWI nchini yameendelea kwa kiasi kikubwa.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amesema maambukizi ya vijana kwa sasa yamefikia asilimia 40 .
"Elimu zaidi inazidi kutolewa.ya kujikinga na virusi vya ugonjwa wa ukimwi kwa makundi yote "amesema.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi nchini (NACOPHA) Leticia Mouris amewaasa mabinti wa kike kutokukubali kurubuniwa na wanaume.
Aidha Leticia amepongeza wakurugenzi wa halmashauri nchi kwa kuboresha huduma za waathirika wa ugonjwa wa ukimwi na kusema kuwa ni jambo.jema .
Hatahivyo mwenyekiti huyo amesema pia kumekuwa na ongozeko la ukatili wa kijinsia kwa wanawake walioathirika na ugonjwa wa ukimwi na kuomba serikali kusaidia kukomesha vitendo hivyo.
0 Comments