Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam
Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amewataka waumini wa dini ya kiislam na watanzania wote kwa ujumla kuendelea kuomba kwa ALLAH (S.W) Ili mvua inyeshe kwa kipimo sadifu kisicho ambatana na madharaja wala maafa.
Akizungumza na waandishi habari Jijini Dar es salaam katika Makao makuu ya BAKWATA, kwa niaba ya Mufti, Msemaji wa Mufti Sheikh Hassan Chizenga amesema Novemba 17 mwaka huu Mufti Mkuu wa Tanzania aliwangiza waumini nchini kufunga siku tatu na kuomba dua kwa wingi kutokana na mvua kuchelewa mno kunyesha nchi nzima .
Aidha, amezitaka hotuba za ijumaa zitakazo tolewa pamoja na Shughuli za kiibada zijikite zaidi katika kumshukuru Mungu, kwani kufanya hivyo Mungu atasikia kilio na kujibu kwa haraka katika kipindi hiki ambacho wema wa duniani ni wachache na uovu umekithiri.
Amesema wito alioutoa wiki iliyopita ulipokelewa na mikoa yote ambapo dua za kumbelembeleza zilifanyika na hatimaye Mwenyezi Mungu aliweza kujibu dua hizo bila ya madhara yoyote.
"Nawaomba waislamu wote na Watanzania kwa ujumla tuendelee kumuomba Mungu atupe mvua hizi kote ambako zimefika na sehemu ambazo bado hazijafika ziweze kufika kwa kipimo sadifu"amesema sheikh Chizenga.
Sheikh Chizenga amesema kutokana na neema kubwa watanzania na waislamu kwa ujumla wanapaswa kutambua kuwa Mungu yupo na ndiye mtawaka wa dunia hivyo yapasa kujipendekeza kwake kwa ibada nyingi kisha kutubu makosa.
"Tukiomba toba kutatusaidia kupata neema nyingi mbalimbali tunazoziitaji katika maisha yetu duniani na kesho Ahkhera"amesema
Ameongeza kuwa, Mungu anasema katika Qurani surat Nuh aya 10 hadi ya 12 anasema na kutuhusia kupitia kinywa cha Nabii Nuhu kwa kusema muombeni msamaha mola wenu katika yeye ni mwingi mno wa kusamehe.
Sheikh Chizenga amesema kitu cha muhimu zaidi katika dua na ibada ni kuzidi kujinyenyekeza kwa Mungu ili azidi kudumisha amani nchini na kuwashika mkono viongozi wa nchi.
0 Comments