Header Ads Widget

WANAWAKE PWANI WATAKIWA KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA

 


WANAWAKE mkoani Pwani wametakiwa kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa kujikomboa nakutokubali kuwategemezi kwa kufanya shughuli za ujasiriamali ili kujikwamua kiuchumi.


Hayo yalisemwa mjini Kibaha na mbunge wa viti maalum wa mkoa huo Dk Alice Kaijage alipokuwa akizungumza na uongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kibaha Mjini na wajisiriamali ambao wanapatiwa mafunzo na Umoja huo wakati wa kuhitimisha sherehe za miaka 60 ya uhuru.


Kaijage alisema kuwa wanawake wanapaswa kujivunia kwa kuchukua hatua na kufuata nyayo za Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akipambana kuwakwamua akinamama na Watanzania kiuchumi.


"Tuwapongeze UWT kwa kutoa mafunzo kwa wajasiriamali kwani kumkomboa mwanamke umeikomboa jamii na unakuwa unamsaidia Rais kuwakomboa kiuchumi,"alisema Kaijage.


Kwa upande wake mwenyekiti wa UWT Kibaha Mjini Eline Mgonja alisema kuwa wametoa mafunzo ya ujasiriamali kwa akinamama bure ili wapate elimu kwani hata katiba inazungumzia kumkomboa mwanamke kiuchumi kifikra na kimawazo.


Mgonja ambaye pia ndiye mwalimu wa mafunzo hayo ya ujasiriamali alisema kuwa darasa limewapa fursa wanawake kutengeneza bidhaa kwa nadharia na vitendo ili kumsaidia Rais ambaye anawapigania wanawake ili watoke kwenye utegemezi.


Alisema kuwa wanawake hao tayari wameshajikwamua kiuchumi kupitia mafunzo ya ujasiriamali ambapo kipaumbele chake kilikuwa ni kutoa elimu bure kwa wajasiriamali na kujenga kitega uchumi na utengenezaji wa vitu mbalimbali kama batiki, mafuta mimea ya asili, mafuta ya nazi mawese, mnyonyo sabuni za kuogea, sabuni za majani ya mlonge mwarobaini na mchele.


Sabuni kutumia mwani usafi shampoo make as ni ya mlenda na ufuta ukitengeneza nywele zinapendeza sabuni ya mlenda ni kitu kipya zamani tulitumia mlenda kuogea sabuni zimethibitishwa na TBS 


Neema kubwa imeshuka hospitali kwa sasa vitanda vingi vya kujifungulia hospitali kila mahali kwenda Dar es Salaam ulikuwa unatumia muda mrefu lakini sasa hadi mwendokasi umeme upo maji yanapatikana walikuwa hawatambuliki wamejitambua ni wasalishaji mali.


Naye mjasiriamali Rehema Sasia alisema kuwa anashukiru uwt kwani sasa anauwezo wa kutengeneza vitu mbalimbali na kujipatia kipato ambapo mwanzo alikuwa hajui chochote.


Sasia alisema wamejifunza kutengeneza baadhi ya vitu ikiwemo Vicks ambayo huwa inatengenezwa nje ya nchi na wamejengewa uwezo wa kujitangaza na wanapata masoko nje ya mkoa.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI