Header Ads Widget

WANANCHI KILIMANJARO WAOMBA BARABARA

 





Wananchi wa kata ya kilema kaskazini wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wameiomba Serikali kukaarabati barabara kutoka marangu mtoni  mpaka maua seminary kwani imekuwa ikipata matengenezo hafifu hali inayosabaisha kumomonyoka pindi mvua zinaponyesha.


Akizungumza kwa niaba ya wananchi mbele ya mbunge wa Jimbo la vunjo Mh.Charles Kimei, Diwani wa kata hiyo Anna Anna Lyimo amesema kuwa kwa kipindi Cha mvua barabara hiyo huaribika na kutofaa kwa matumizi.


Amesema kuwa wamekuwa wakiteseka hususani pale wanapotoka katika shughuli mbalimbali kwani  magari yamekuwa  yakiwashusha wananchi  katika eneo la kilema kati na kutembea kwa miguu mpaka kufika Rua.




Mbunge huyo amesema kuwa Serikali imeweka mikakati ya kutatua chanagamoto zinazowakabili wanchi wa Jimbo hilo ikiwemo ubovu wa vyoo vya wanafunzi  barabara pamoja madarasa.


Amesema kuwa katika kuhakikisha changamoto hizo zinatatuliwa anafanya mazungumzo na Wizara husika ili kuangalia Kama Kuna uwezekano wa kutatua kero hizo.



Kwa upande wake katibu wa chama Cha Mapinduzi wilaya ya Moshi vijijini Ramadhan Samwel Mahanyu amesema kuwa azifuatilia fedha zote zinazokusanywa na baadhi ya viongozi na kudai kuwa zinaenda kwenye matumizi ya barabara lakini hazifanyiwi kazi hiyo iliyokusudiwa.


Hata hivyo Mh.Mbunge wa Jimbo hilo la vunjo yupo katika  ziara ya kusikiliza kero za wananchi wake katika kata zote ili kuangalia ni namna gani ya kuweza kuzitatua na kuzitafuta ufumbuzi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI