Header Ads Widget

WADAU WA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA WAKUTANA DODOMA




WADAU  wa kupinga Ukatili wa Kijinsia wamekutana jijini Dodoma huku mashirika na Asasi za Kiraia mbalimbali kutoka mikoa 13 ya Tanzania bara na Moja kutoka Zanzibar kujadili Mpango Wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA).


Akiongea na kituo hiki leo jijini hapa Afisa Programu kutoka Idara  ya Habari mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Jackson Malagalila amesema wamekuwa na asasi hizo na kufanya nao kazi taangia  mwaka 2017.


 "Lengo lao kuwa na asasi hizi ni kujadili kwa pamoja  mpango wa taifa wa kukomesha ukatili dhidi ya wanawake na Watoto unaokwenda kutekelezwa na mashirika kwa kufanyakazi na serikali kuhakikisha  tunatokomeza vitendo hivi vya kikatili," amesema Mawangalila  .


 Aidha amesema wamefanya Tathimini ya hali ikoje na imeonekana wazi kuna hatua imepigwa hasa katika uelewa na kuanzishwa kwa madawati ya kijinsia kamati za MTAKUWWA zinazidi kuanzishwa licha ya kuwepo kwa changamoto ambazo zinatakiwa kufanyiwa kazi ikiwemo ufuatiliaji wa rasilimali zinazotengwa kwa ajili ya kufuatilia MTAKUWWA  na ni jinsi gani serikali inasimimia kwa madhubuti fedha zinazotengwa kwa ajili ya usimamizi huo wa MTAKUWWA  zinakwenda kufanya kazi iliyokusudiwa.



Naye Tatu Mrutu ambaye anafanyakazi na shirika la JISO  lililopo Mkoani Kilimanjaro na mwanasheria amesema kunahaja ya wabunge ambao ndio wawakilishi wa wananchi kubadilisha sheria kandamizi.


Amesema ni kweli bado zipo sheria  kandamizi ambazo zinakwenda tofauti na sheria ya mtoto ya mwaka 2007 kama sheria ya ndoa na sheria na mirathi ambazo zinaenda tofauti na katiba ya nchi.


"Wabunge ambao wao ndio watunga sheria hiyo sasa wanatakiwa wadilisha sheria hizo kwani zimekuwa zikiwapa wakati mgumu  wao kama wana harakati wa kupinga ukatili wa kijinsia hasa katika masuala mazima ya kuamua kesi mahakamani.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI