Header Ads Widget

MIFUMO MIZURI YATAKIWA KUANDALIWA ILI KUWASAIDIA WAKULIMA KUWEZA KULIMA KILIMO CHENYE TIJA

 



TUME ya Maendeleo ya Ushirika  imetakiwa kutengeneza mifumo mizuri itakayowasaidia wakulima kuweza kulima kilimo chenye tija ili kuondokana na umasikini kwani karibu ya wakulima wote hapa nchini ni masikini kutokana na mifumo iliyowekwa haiwatengenezi wakulima kuwa tajiri.


Sambaba na hilo amesema kuwa inasikitisha sana kuona ushirika kuchukuliwa kama chombo cha ubabaishaji na sehemu ya kupigia pesa  kwani taswira ya nje ushirika unaonekana ni ujambazi


Hayo ameyasema  jijini hapa na Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wakati akifungua mafunzo ya shirikisho la vyama vya ushirika (TFC)  ambapo vyama vya ushirika wa mazao - AMCOS vimetakiwa kuanzishwa vyama vya ushirika wa akiba na mikopo SACCOS 

huku akisema ni wakati sasa wa vyama vya ushirika kutengeneza mifumo ya kibenki ili pesa za wakulima zisiliwe kiholela.


"Ni ukweli usiopingika sekta ya kilimo ndio sekta ilioajili watu wengi kwani asilimia 60 ya wananchi wamejikita huko kwenye kilimo hivyo tuwakombee wakulima katika umasikini waliokuwa nao hivi sasa," amesema Bashe.


Kwa upande wake Collin Nyakunga Mrajisi Msaidizi Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania mafunzo  hayo yanalenga kujifunza uandishi wa maandiko ya ufadhili wa miradi inayofadhiliwa na ASDP .


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI