Wataalam wa Utafiti wa Madini kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzani (GST) wamefanikiwa kutoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa Madini zaidi ya 300 mkoani mwanza......Na.Samwel Mtuwa - Mwanza.
Mafunzo hayo yalianza rasmi Novemba 26,2021 na kuhitimishwa Disemba 1, 2021 kwa kuwashirikisha wachimbaji kutoka maeneo mbalimbali ndani ya wilaya ya misungwi kama vile maeneo ya Shilalo, Mwamazengo , Lishokela na Chatta.
Lengo kubwa la kutoa mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo na uelewa wa namna bora ya uchukuaji wa sampuli wakilishi kutoka katika maeneo ya kazi Kwa ajili ya uchunguzi wa maabara.
Kufanyika kwa mafunzo hayo katika njia ya nadharia na vitendo kumeweza kuwaelimisha wachimbaji wengi walioudhuria ikiwa pamoja na viongozi wa vikundi mbalimbali vya wachimbaji wadogo mkoani mwanza.
Mpaka taasisi ya GST tayari imefanikiwa kutoa mafunzo Kwa wachimbaji wadogo wa Madini katika mikoa kumi.
0 Comments