Header Ads Widget

UVCCM TAIFA WAMVAA JOB NDUGAI


Katibu mkuu wa Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM)Taifa Kenani Kihongosi akizungumza na wananchi wa Kihesa mjini Iringa baada ya kukagua ujenzi wa madarasa shule ya Sekondari Kihesa  ,kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Moyo na mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Iringa mjini Salvatori Ngerera 


KATIBU mkuu  wa  jumuiya  ya umoja  wa  vijana  wa  chama  cha  mapinduzi (UVCCM) Taifa  Kenani Kihongosi amesema  wapo  baadhi ya  viongozi wameanza  kutoa matamko ya kumkwamisha  Rais Samia Suluhu Hassan  katika  kuliletea Taifa maendeleo kuwa  wao kama  vijana  watahakikisha kabla ya  Rais hajakwama  viongozi hao  watakuwa  wamekwamishwa  wao .

Kuwa  watambua  mikopo  ni sehemu ya maendeleo na  hata nchi kubwa zimekopa na hata  wabunge wanayo mikopo mbali mbali ambapo  si  kosa ila ndani ya  siku chache wameibuka  viongozi  wanaoheshimika kwenye  Taifa wameenda mbali  wanakosoa na kuona  mikopo  hii haina  tija jambo ambalo  si sawa .

Akizungumza Leo  mjini  Iringa  baada ya  kukagua  ujenzi  wa  vyumba  vya  madarasa  katika  shule ya  sekondari  Kihesa  ujenzi unaotekelezwa  kwa  fedha  zilizotolewa na serikali  ya awamu ya  sita  chini ya  Rais  Samia ,Kihongosi  alisema kuwa  mbali ya kazi kubwa inayofanywa na Rais  samia katika    ujenzi wa miradi mbali mbali  wapo  baadhi ya  viongozi wanaibuka na kupinga .

Alisema kuwa  tangu   Rais Samia aingie madarakani  mwezi  machi mwaka  2021  kumekuwepo na  jitihada  kubwa  zenye mageuzi makubwa katika  Taifa  na maendeleo makubwa  kwa  kuwepo kwa mambo makubwa ambayo yamefanyika kwa kipindi  cha miezi tisa  aliyokuwepo madarakani   na  kila  mmoja ni shahidi kwa kazi  hiyo.

“Deni  la taifa  linakaribia  shilingi Tirioni 70  Lakini  tutambue  kuwa deni  la serikali ya  awamu ya  sita  imekuwa  ni serikali  yenye uwazi  zamani ya kwanza  hadi  ya tano  fedha  zilikuwa  zikikopwa  lakini  uwazi  ulikuwa hauwekwi  wazi  wala wananchi  mlikuwa hamuelezwi  serikali  imekopa  nini na imefanyia  nini lakini Mheshimiwa  Samia  amechukua  fedha  Trilioni moja  na  bilioni miatatu  fedha ambazo baada ya  kuzipata  ameshirikisha  bunge  na  viongozi wa  serikali  pamoja na kufanya kikao  kueleza matumizi ya  fedha  hizo  watanzania  wote  waliona  na  hili jambo la  mfano na la kupongezwa “  alisema  Kihongosi

Kuwa  iwapo  kiongozi  mkuu wa nchi anaweza  kuchukua  fedha na kuainisha  matumizi yake  kwa  mwananchi  anajua  wazi kuwa  fedha  iliyokopwa inakwenda  kufanya nini .

Alisema  faida ya  mikopo  huo  ni kuwa hakuna riba  yoyote kwa  serikali na  ni  deni litakalolipwa kwa zaidi ya miaka  20  tena  pasipo  riba  yoyote  ile na  fedha  hizo  zimesambazwa  kwenye ujenzi  wa  vyumba  vya madarasa na  sekta ya afya  ,maji  na maeneo mengine kila mkoa.

Pia  alisema  fedha  hizo  zimeelekezwa  kwenye   uboreshaji wa  miundo mbinu ya  barabara kila kona ya  nchi  hii .

Aidha  alisema kwa  kipindi  kifupi cha  serikali ya  wamu  ya  sita madarakani  fursa  nyingi  zimekuwepo  kila  eneo  ambapo kwa  vijana  wa  vyuo  vikuu  kwenye  kipindi  cha  serikali  hii  ndipo  walipopata  mikopo  zaidi  kuliko  wakati  mwingine wote kwa  mikopo zaidi ya  bilioni 570  .

Alisema  kuwa  kwa  miradi  inayoendelea  nchini  ni  miradi  itakayonufaisha vijana  wengi  zaidi na  wao kama  vijana  hawatakubali  kuona  kuna   viongozi  wanatumia vyombo  vya habari  kutaka  kumkwamisha Rais kwa  kumsema  vibaya kwa  viongozi hao kabla ya hawajafanikisha  kumkwamisha  Rais  watakwamishwa  wao maana  yeyote anayesimama na kumpinga Rais  kwao ataonekana ni adui ni lazima ashughulikiwe .

  Iwapo  wewe  ni kiongozi  ndani ya  nchi  hii  ama  kiongozi ndani ya  chama  una  hoja  ya  kumshauri  Rais  ni  vema  kutumia  vikao husika  kufikisha  ushauri  wako  kuliko  kwenda  kwenye  vyombo  vya habari ama  kutumia majukwaa  ya nje  kumsema  vibaya  kiongozi huyo hatavumiliwa hata kigodo .

Wakati  huo  huo  Kiongosi  alisema   kuwa  pamoja na  jitiahda  za  kuendelea  kupamoja na miradi ya maendeleo  Rais Samia ameendelea  kufungua milango ya  utalii kwa  kulitangaza Taifa  kupitia Filamu ya  The  Royal  Tour .

Aidha  alisema  kuna  baadhi ya maeneo  wamekuwa  wakiandika kwenye vyumba  vya madarasa yanayojengwa  kwa  fedha  za mikopo kuwa  miradi ya UVIKO 19 kuwa  kufanya  hivyo ni  kosa na tayari katibu mkuu wa CCM Daniel  Chongolo alipiga marufuku maana  fedha  hizo ni mikopo ambayo inapaswa  kurejeshwa na  sio fedha  za UVIKO 19.

Alisema mtu  unapokopa  fedha matumizi ni  juu yako  na  mkopeshaji  hakupangii matumizi ya  fedha  anazokukopesha  na hivyo  fedha  zinazojenga  madarasa ni  fedha na  mkopo  sio miradi ya UVIKO 19.

Awali  mkuu  wa  wilaya ya  Iringa Mohamed  Moyo alieleza  hatua  mbali mbali  ambazo  wilaya ya  Iringa  imefikia  katika  ujunzi wa vyumba  vya madarasa na  kuwa  wilaya ya  Iringa na  mkoa wanategemea January 17  wanafunzi  wote  wataanza masomo  kwani miradi   ya ujenzi  wa vyumba  vya madarasa imefika hatua ya mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI