Mwenyekiti wa chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam Kate Kamba ameipongeza Wilaya ya Ubungo kwa kukidhi vigezo katika mradi wa Shule za Sekondari zilizojengwa kwa kutumia pesa za Uviko 19 katika maeneo mengi nchini Tanzania......Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam
Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua katika Mkutano Mkuu wa umoja wa Vijana (UVCCM) Kata ya Mabibo ambapo amesema hatua hiyo imekuja kutokana na Umoja na mshikamano baina ya viongozi na wakandasi waliokabidhiwa kazi hiyo.
"Naomba muendelee hivi hivi mulivo mumefanya kazi kubwa sana katika mradi huu, katika mkoa wa Dar es Salaam, Wilaya ya Ubungo mmekua vinara mmekidhi vigezo vyote vilivyokua vikitakiwa katika mradi huu"amesema Kate.
Aidha, akijibu suala la ukosefu wa ajira kwa vijana katika Kata hiyo, amesema atakua nao bega bega kuhakikisha vijana wanaweza kujiajiri wenyewe kwa kubuni mradi wa maendeleo utakaoweza kuwapatia tija na kipato.
"Katika kila Halmashauri kuna pesa zinazoletwa asilimia 10 kwa ajili ya vijana, akina mama na walemavu, kuna sehemu niliona mradi vijana wameanzisha nataka niwachukue vijana hapa niwapeleke muende mukajifunze kama mutaupenda muufanye katika kiwango kizuri zaidi kupitia pesa hizi za Halmashauri"amesema Kate.
Hata hivyo, amewataka vijana kutotumika kisiasa na badala yake wachague viongozi ambao ni sahihi na wanauwezo wa kuongoza, kuwavusha sehemu moja kwenda nyengine kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi ya Tanzania.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mabibo Joseph Thomas amesema kata hiyo imepokea fedha za UVIKO 19 millioni 160 kutoka Serikali kwa ajili ya Ujenzi wa Madarasa 8, ambapo madarasa hayo yamejengwa kwa vigezo vilivyokua vinahitajika.
Amesema kuwa, Kata ya Mabibo ni moja ya kata 14 zilizoko katika Manispaa ya Ubungo na kueleza kuwa fedha hizo walizopata zimekuja kwa maelekezo ya kutumika kwa wakati.
Aidha amesema awali darasa moja lilikuwa likibeba wanafunzi 100 hivyo baada ya Ujenzi wa Madarasa hayo kukamilika itasaidia kupunguza msongomano wa wanafunzi.
Naye, Katibu UVCCM Kata ya Mabibo Raufu Mkonga amesema kuwa, lengo la UVCCM ni kuhakikisha wanaongeza jeshi kubwa la wanachama katika mapambano ya kuilinda na kuitekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa vitendo.
Aidha, amesema wanatamani wawe na mradi wa kwao ambao itawezesha kuwasaidia kujiajiri na kupata kipato,kwani suala la ajira imekua changamoto kubwa sana hususani kwa vijana.





0 Comments