Mbunge wa MalinyI akizungumza na wananchi
TAARIFA YA MBUNGE WA MALINYI MHE ANTIPAS Z. MGUNGUSI JUU MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI HALI ILIYOSABABISHA MKULIMA MMOJA KUUWAWA
Wilayani Malinyi mkoa wa Moro tangu juzi tarehe 27.12.2021. kumekua na machafuko ya usalama, mauji na majeruhi baina ya wakulima na wafugaji, ambapo ilianza kwa wafugaji kuingiza mifugo kwenye mashamba ya wakulima, Katika skimu ya umwagiliaji, ambapo ng'ombe waliingizwa na kuendelea kula na kuharibu mazao.
Wakulima waliokuwa maeneo yao na kujaribu kukemea kuzuia uharibifu ,hali ambayo wafugaji walianza kuwashambulia na kumuua mkulima mmoja na kuwajeruhi wengine kadhaa na Maiti ilipatkana alfajiri saa 9.
Tarehe 28.12.2021, Askari Polisi walienda eneo la tukio Kijiji Cha Alabama kata ya Itete kwa ajili ya kuchukua mwili huo kwa ajili ya postmodern, jambo ambalo wananchi hawakuafiki kwa madai kuwa wamekua wakionewa na wafugaji na hawaoni jitihada za dhati ya polisi na serikali ya huku kuwasaidia kilio chao cha Kila siku Sasa wanachukua mwili kuchunguza nini wakati wanajua kapigwa na kuvunjwa uti wa Mgongo sehem ya juu kwa kupigwa na kitu kizito hadi kufa? Hiyo ndio ilikua hoja ya wananchi.
Polisi walihitaji kuchukua mwili kwa nguvu hali ambayo ilizua taharuki, na Askari Polisi walianza kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya watu, lakin hawakufanikiwa kutokana na misimamo ya wananchi hadi askari wakakata tamaa.
Mwili wa marehemu ulisafirishwa na wanafatilia kwenda ifakara kwa mazishi.
Mimi nilipopata taarifa jana nikitoka dodoma na kuingia Malinyi ucku.
Jana asubuhi tarehe 29.12.2021 nilianza kikao na DC na wasaidiz wake ambapo walinipa taarifa fupi ya hali halisi( ofisini kwa DC) baada na kikao Cha ndani na Viongozi wa vijiji, vitongoji na ambapo pamoja na mambo mengine kikao hicho na wataalam wa ulinzi walinishauri kutofanya mkutano wa hadhara kwani, hali ya usalama haikuwa shwari, wao walidhan kutakuwa na machafuko Zaid, ili kukiwa na mikusanyiko, hivyo tuache hadi siku za usoni hali ikipoa
Ushauri huo sikuukubali, kutokana na mambo mengi, ikiwemo kuwa wananchi wenzangu mimi ni mwakilishi wao, na ni mwenzao, sikupaswa hata siku moja kuwaogopa kuwafikia kuwapa pole, kutoa faraja, majawabu na mwelekeo za sakata Zima. Wasiposikilizwa, wangeenda kusema wapi waliyonayo moyoni? Nami kama Mbunge iweje katika Kipindi kigumu kama hiki niwe mbali nao, ili hali kipindi chote cha magumu mengine ya masika na mafuriko nilikua pamoja nao muda wote kuleta suluhu.
Nikaamua kufanya mkutano mkubwa wa hadhara, na nikiri wananchi kuwa wengi sana kuliko mikutano ya kawaida ya siasa za maendeleo Wilayani Malinyi.
Pamoja na mambo mengine, wananchi( wengi wao walikua wakulima) karibia wote waliiongea kwa niaba ya wenzao, wakilalamika sana kuwa wamekua wakionewa mara kwa mara kwa Mazao yao kuliwa na hawakuona jitihada za dhati za serikali kwa wao kusaidiwa kumalizwa tatizo hili. Hivyo walisema watachukua hatua wao wenyewe kujitetea bila kujali kama serikali ipo.
Nilizingumza nao sana, na mwisho kuwahakikishia kwamba mimi mwakilishi wao, nitavalia njuga jambo hili, na kutaka kulimaliza ili Amani ya kudumu irejee.
Kiujumla, wananchi wenzangu nami kama mwakilishi wao, tunaisisitiza serikali kufanya jitihada zote, kuwabaini Waanzilishi wa tatizo ili mwishowe Sheria ichukue nafasi yake.
Nikiri kuwa mkutano ulikua mgumu sana kutokana na watu kuwa wengi na wenye hisia Kali na hasira, lakini nilifanikiwa kuwekana nao sawa, na ni kweli kuwa nitashughulikia jambo hili kwa nguvu zote.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Martin Shigella alifanya sehemu kubwa kuhakikisha wananchi wanakuja na Amani na wanarudi katika hali ya kawaida kupitia mkutano ule, kwanza aliunga mkono mpango wangu wa kulazimisha kufanyika kwa mkutano wa hadhara pamoja na Mazingira yaliyokuwepo, na Alionbea na wananchi katika mkutano ule kupitia simu yangu kwa Loud Spika, alitoa maelekezo na kuahidi wiki ijayo yeye atafika Malinyi kwa ajili ya mkutano na wananchi, kwani Sasa anamalizia msiba wa mama yake.
Migogoro wa wakulima na wafugaji wilayani Malinyi, Sasa imekua sugu , katika mikutano yangu ya vijiji kwa vijiji , 96% ya vijiji vyote wananchi wanalalamikia jambo Hilo.
Wananchi wa Malinyi, tunahitaji uwepo wa mifugo na kilimo, jamii zote mbili wakulima na wafugaji ni zetu na ni lazima kuishi kwa pamoja. Tatizo ni kwa baadhi ya wanajamii hii hasa wafugaji ambao hawazingatii taratibu za adabu na kuishi kwa udugu, hao tutahangaikia nao kwa utaratibu na Sheria, kuhakikisha wanaishi kwa NIDHAMU na Amani.
Ukorofi, haufanywi na Kila mfugaji, wapo wastaarabu wenye nidhan, Lakini wale wakorofi kwa Sheria na taratibu zetu tutahangaikia nao.
Mini sio muumini wa kulipana fidia, sababu kwanza fidia sio halisi na hazikidhi, pili, ulipaji fidia unalea ujeuri kwa wenye vipato kukoleza chuki na mapigano.
Tunakwemda kufanya sensa madhubuti, kuona Kila mwenye mifugo, aoneshe ukubwa Wana eneo analomiliki kihalali katika Kijiji chake.
Ikitokea mtu anamifugo mingi nasi aoneshe eneo kubwa analomiliki, kama Hana, ni dhahiri mtu huyo anaenda kusababisha migogoro.
Nitafanya mkutano wa hadhara na Wananchi katika kuweka hali sawa.
Mhe. ANTIPAS MGUNGUSI Mbunge jimbo MALINYI





0 Comments