Header Ads Widget

UTT AMISS WAFANYA VIZURI, WAWEKEZAJI WAOMBWA KUJITOKEZA

 






Watanzania wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika mifuko ya uwekezaji kwa pamoja (UTT AMISS) Ili waweze kupata faida kutokana na utendaji kazi wa uwendeshaji wa mifuko hiyo.......Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam


Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa UTT AMISS, Simon Migangala wakati walipokua kwenye mkutano wa mwaka ambapo utafanyika siku mbili katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalim Julius Nyerere.


"Leo ni siku muhimu sana kwetu, kwani sheria na kanuni zinatutaka tukutane na wawekezaji mara moja kwa mwaka, tuna mifuko sita "amesema Simon.



Aidha, amesema kuwa, wameongeza matawi katika mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza, Arusha ambapo mfuko wa umoja ni miongoni mwa mifuko hiyo ambayo imefanya vizuri ambapo katika asilimia 50 wamewekeza katika hisa na asilimia 50 nyengine imewekeza katika hati fungani.


Aidha, amesema kuwa wameweza kuvuka malengo waliojiwekea ya miaka miatano kutoka mwaka 2019 hadi mwaka 2024 ambapo wamevuka malengo hayo kwa miaka miaka miwili.


Hata hivyo, amesema wameboresha utoaji wa huduma zao kwa wateja ambapo wamefungua app ya UTT AMISS inayowawezesha wateja kupata taarifa zote za mifuko.



Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodi UTT AMISS Casmir Kyuki amesema mifuko hiyo imeweza kufanya vizuri  kutokana na elimu walioitoa kwa kuzunguka katika maeneo mengi nchini Tanzania.


"Tumetoa elimu na tumewafikia watanzania wengi ambapo mwanzo tulikua kwenye mikoa mikubwa ikiwemo Dar es Salaam ila kwa sasa tumefika hadi wilayani watanzania wametuelewa"amesema Kyuki.


Amesema kuwa, mifuko hiyo inasimamiwa na wataalamu ambao wamepatiwa mafunzo hivyo watanzania wajitokeze kwa wingi Ili wawekeze kwani pesa zao zipo sehemu salama.


"Kwa kweli Mungu ni wa ajabu sana tumepata mafanikio kipindi ambacho kulikua kigumu kiuchumi na kibiashara kutokana na ugonjwa wa UVIKO 19, lakini kwa mfuko tumefanya vizuri mno"amesema Kyuki.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI