Wazazi wametakiwa kuhakikisha wanawapeleka watoto shule ili wapate elimu sahihi ambayo itawasaidia katika maisha yao ya badae pasipo kuangalia matokeo hasi kwa watoto....Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Akizungumza katika mahafali ya 25 ya kuhitimu masomo ya awali kwa watoto wa shule ya awali iitwayo Castor Sekwa inayomilikiwa na kanisa la mama mwenye hurumu lililopo Ngokolo mjini Shinyanga mgeni rasmi Bwana France Matunu amesisitiza kuwa ni wajibu wa wazazi kuhakikisha watoto wanapata elimu yenye ubora.
Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Sr. Venansia Mtamizi amesema siri kubwa ambayo wanafunzi wanapaswa kuitumia katika safari yao ya masomo ni uvumilivu, usikivu, utii kwa kuwaheshimu wazazi pamoja na walimu.
“Siri kuwa wanayohitaji sana kuitumia katika masomo ni kuwa na usikivu na utii kwa wazazi na walimu daima wapende kujua mambo mbalimbali wanayofundishwa na walimu na wapende kujiendeleza katika nafasi mbalimbali katika masomo yao”
Wakizungumza baadhi ya watoto waliohitimu masomo ya awali katika shule hiyo wamemshukuru Mungu, wazazi pamoja na viongozi mbalimbali wa dini akiwemo paroko wa kanisa la mama mwenye huruma ambaye pia ni meneja wa shule hiyo Padre Adolf Makandagu.
Aidha Jumla ya watoto 61 wamehitimu masomo ya awali katika shule hiyo ya Castor Sekwa huku wavulana 31 na wasichana 30 ambao wote wanatajajia mwaka ujao 2022 kuanza kusoma darasa la kwanza.
0 Comments