Header Ads Widget

TOFAUTI YA PhD NA HONORIS



Media nyingi zimekua zikifanya makosa kama waliofanya TBC leo, kuchanganya Shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD) na shahada ya Udaktari wa heshima (Honoris causa/doctorate).


Shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD) inasomewa darasani, inafanyiwa utafiti, na utafiti huo unatetewa kwenye jopo la maprofesa. Lakini Shahada ya udaktari wa heshima inatolewa bila kusomewa. Inatolewa kwa mtu yeyote aliyefanya jambo kubwa lililogusa jamii.


Bodi ya chuo inakaa na kuangalia mtu aliyefanya jambo kubwa kwa jamii wanamtunuku shahada ya udaktari wa heshima kama njia ya kutambua mchango wake. Chuo kikuu UDSM, idara ya sanaa (FPA) inaweza kumtunuku Diamond shahada ya udaktari wa heshima kama njia ya kutambua mchango wake ktk kukuza sanaa yetu kupitia muziki.


Udaktari wa Falsafa (PhD) na udaktari wa heshima (Honoris causa) ni vitu viwili tofauti kabisa. Havina uhusiano hata kidogo. Moja ni academia na nyingine ni just honorarium.


#Swali1: Je kuna shahada za udaktari wa aina ngapi?


Jibu1: Zipo nyingi. Kwa uchache kuna shahada ya udaktari wa binadamu (MD), udaktari wa falsafa (PhD), udaktari wa Sheria (LLD), Udaktari wa sheria za kanisa (JCD), udaktari wa heshima (Honoris Causa) Mbunge Ritta Kabati na Kuna baadhi ya wanahabari na watu wengi mashuhuri 


Swali2: Je nawezaje kuzitofautisha?

Jibu2: Inatakiwa kwenye mabano kuweka initials. Kwa mfano Dr.Benson Bagonza (PhD), Dr.Chris Cyrilo (MD), Dr.Wilbroad Slaa (JCD), Dr.Seng'ondo Mvungi (LLD) au Dr.Jakaya Kikwete (Honoris causa).


#Swali3: Je mtu mwenye udaktari wa heshima anaruhusiwa kuanza na Dr kwenye jina lake?


#Jibu3: Inaruhusiwa japo sio jambo la kuendekeza sana. Wengi wametunukiwa udaktari wa heshima na hawajiiti Doctors. Bill Clinton alitunukiwa mara 3 lakini hajawahi kujiita doctor. Mwal.Nyerere alitunukiwa mara 8 na vyuo mbalimbali vyenye hadhi lakini hakuwahi kujiita Dr.Nyerere.


Juzi mshambuliani wa Man U, Marcus Rashford ametunukiwa shahada ya udaktari wa heshima na Manchester University, moja ya vyuo vikubwa sana duniani, na hajiiti Dr.Rashford.


Lakini Afrika tunapenda sana utukufu. Mtu akitunukiwa udaktari wa heshima na Mchambawima University, kesho yake utasikia "naitwa Dr.Makoroboi Vuai Makaratasi" anaongeza na neno PhD mwishoni. Ulimbukeni tu.!


Mchambuzi ni Malisa GJ

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI