Halmashauri ya Meru kupitia chuo cha maendeleo ya jamii kimeanza matembezi kuhamasisha wananchi kujitokeza katika zoezi la chanjo la uviko 19 pamoja na kupima magonjwa yasiyoambukiza na yanayoambukiza kwa lengo la kufahamu hali ya afya zao.......Na Teddy Kilanga_ Arusha
Akizungumza katika hospitali ya wilaya ya Meru Tengeru,desemba 7,2021,kwa niaba Mkuu wa wilaya ya Arumeru,katibu tawala wa wilaya hiyo,Mwalimu James Nchembe amesema matembezi hayo yanaenda sambamba na mafunzo ili jamii ifahamu namna ya kujikinga magonjwa hayo na kutumia lishe sahihi.
"Kama tulivyosikia kupitia mafunzo yaliyotolewa na wataalam wa afya wa halmashauri ya Meru kuwa UVIKO-19 na magonjwa sugu yasiyoambukiza na yale yanayoambukiza jinsi yanavyodhorotesha shughuli mbalimbali za maendeleo,"amesema Katibu Tawala huyo.
Aidha amewasisitiza wananchi wa wilaya hiyo kupima afya zao mara kwa mara pamoja na kupata chanjo kwani ni njia kuu kuzuia kuenea kwa maginjwa hayo.
Kwa upande wake Mganga mkuu wa halmashauri ya Meru,Dkt.Maneno Focus amesema wamekuwa wakishirikiana na chuo hicho katika kuhamasisha jamii jamii juu ya kupima magonjwa hayo na kutoa elimu ya uviko ikiwa hadi sasa wameshawafikia vijana takribani 225.
"Katika halmashauri ya Meru hadi sasa chanjo za awamu ya kwanza zipatazo 6000 zimeisha na sasa wapo katika awamu ya pili ambazo wameshachanja watu wapatao 4500 kati ya 5000,"amesema.
Naye Mkuu wa Taasisi ya TICD,Bakari George amesema katika kuadhimisha wiki ya maendeleo ya jamii watakuwa wakijishughulisha na matukio mbalimbali ikiwemo masuala ya ujasiriamali kwa wanafunz.
"Kauli mbiu ni afya bora kwa maendeleo ya jamii ambapo maadhimisho hayo yanatarajiwa kufungwa Desemba 11,2021,"amesema Mkuu huyo .
0 Comments