Header Ads Widget

DKT. MWINYI AONGOZA MKUTANO KWA NJIA YA MTANDAO

 


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi afanya mkutano kwa njia ya Mtandao wa Zoom kuzungumzia mada isemayo “Falsafa ya Uchumi wa Buluu kwa Maendeleo ya Tanzania”. 


Mkutano huo umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, wakiwemo Mawaziri, Viongozi wa Taasisi za Serikali na Sekta Binafsi pamoja na Wananchi kwa Ujumla.


Katika Mkutano huo Dkt Mwinyi ameeleza kwa Kina Sera ya Uchumi wa Buluu na kwa namna gani ambavyo Wananchi wa Zanzibar pamoja na Serikali watanufaika nayo.


Aidha Dkt Mwinyi atumia Mkutano huo kutoa Wito kwa Wawekezaji wa ndani na Nnje ya Nchi, Sekta Binafsi, Wafanyakazi wa Serikali pamoja na Wananchi kwa ujumla kushirkiana na Serikali katika kutekeleza Sera ya Uchumi wa Buluu kwa Maendeleo ya Wananchi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI