Rais wa chama cha mawakili Tanzania,Prof.Edward Hoseah amempongeza Mkurugenzi mkuu wa mashtaka nchini(DPP) Sylvester Mwakitalu kwa kuyaondoa baadhi ya mashauri mahakamani......NA TEDDY KILANGA_ARUSHA
Akizungumza Jana ,Disemba 8,2021 katika mafunzo ya mawakili yaliyofanyikia mkoani Arusha,Prof.Hoseah amesema DPP amejitahidi kwani amefanikiwa kuondoa baadhi ya mashauri mahakamani hivyo anampogeza kwa utendaji wake kazi.
Prof.Hoseah amesema ushauri wao kama Mawakili ni kwamba ni vyema wakazingatia kutopeleka kesi mahakamani kama hazina ushahidi kwani hali hiyo itapunguza mrundikano wa mashahuri mahakamani.
"Pamoja na hayo sisi kama Mawakili wiki hii yote tumeanza na anuai za kitaaluma pamoja na kutoa mada mbalimbali ikiwemo sheria zinazohusu utakatishaji fedha pamoja na uhujumu uchumi ikiwa lengo ni kuona ni kwa namna gani sheria zinavyosadifiana na mikataba ya kimataifa,"amesema Prof.Hoseah.
Amesema katika nchi ya Tanzania utakatishaji fedha ni kosa kubwa ambavyo kupitia sheria mtuhumiwa hupewa adhabu hivyo wameweza kujifunza mambo hayo na ikiwa kama wanasheria wanao wajibu wa kutoa taarifa kwa makosa hayo.
Awali Mwezeshaji wa mafunzo hayo,Wakili Silvia Mwanga amesema lengo ni kutoa elimu kuhusu sheria ya ukusanyaji kodi na masuala ya utakatishaji fedha ambayo yamekuwa bado ni tatizo kwa upande wa wananchi na baadhi ya wanasheria.
Aidha amesema kutokana na uelewa mdogo wa masuala ya utakatishaji fedha bado kuna haja ya kuendelea kupewa mafunzo ya kila mara ili kuwa katika nafasi nzuri yakuweza kuyasimamia vyema.
"Tutaendelea kutoa mafunzo yakiwemo masuala ya ndoa ili kusaidia kufahamu sheria zake katika kuwajengea mawakili uwezo ya kuwa kwenye nafasia nzuri katika kusaidia jamii pamoja na mahakama kufikia masuala ya haki kwa kila mtu,"amesema Wakili huyo.
0 Comments