TIMU ya soka ya mkoa wa Pwani imeifunga timu ya soka ya Dar es Salaam kwa magoli 3-2 kwenye mchezo wa Samia Taifa Cup.
Pwani iliwafunga wenyeji wa mashindano hayo ambapo mchezo ulichezwa leo asubuhi kwenye uwanja wa Duce Jijini Dar es Salaam.
Magoli ya washindi yalifungwa na Selemani Sonzo(Mbape) na Abby Mikimba ambaye alifunga magoli mawili.
Kwa matokeo hayo timu za mkoa wa Pwani za Mpira wa Miguu na Mpira wa Pete zimetamba baada ya kupata ushindi dhidi ya washindani wao kwenye michuano hiyo.
Upande wa mchezo wa mpira wa Pete Pwani ilitamba kwa kuifunga Geita kwa magoli 52-31.
Meneja wa timu ya soka ya Pwani Simon Mbelwa amesema kuwa kutokana na ushindi huo anaamini vijana wake watafanya vizuri kwenye michezo ujao.
Mbelwa amesema mchezo wao utakaofuata watachuana na Kaskazini Pemba kutoka Zanzibar.
Mwisho.
0 Comments