Header Ads Widget

JAKAYA KIKWETE ATOA KAULI HII


Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Ijumaa 10 Disemba 2021, alikuwa  mgeni rasmi katika tamasha la Vya Kale ni Dhahabu lililohusisha wasanii wa zamani wa muziki wa Taarab ambapo amewashauri waandaaji wa tamasha hilo kuifanya tarehe 10 Disemba kila mwaka kuwa siku ya Tamasha la Muziki wa Taarab nchini. 


Rais Mstaafu Kikwete amebainisha kuwa  kinachowavutia wengi kuupenda muziki huo wa Taarab ni kwa sababu unaburudisha na unabeba ujumbe mzuri wenye mafunzo mengi kwenye jamii.


Pamoja na mambo mengine katika tamasha hilo Rais Mstaafu kikwete alikabidhi Tuzo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan Kwa kutambua mchango wake katika kukuza Muziki huo.


Aidha viongozi wengine mbali mbali ikiwemo Rais Mstaafu Kiwete, wasanii wakongwe na watu  mashuhuri walikabidhiwa TUNZO hizo kuthamini mchango wao katika fani hiyo.


Katika hafla hiyo iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City, viongozi mbali mbali walihudhuria akiwemo Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, wabunge na pamoja na watu mashuhuri. 









Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS