Header Ads Widget

BAZECHA JIMBO LA ARUSHA MJINI WAOMBA MARIDHIANO YA PAMOJA NA RAIS SAMIA


Baraza la wazee wa Chama cha demokrasia na maendeleo chadema(Bazecha) jimbo la Arusha mjini wamemuomba Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kukaa pamoja katika kujadili mustakabali wa  kuondoa tofauti zao za vyama vya kiasa na kuwa kitu kimoja.Mwandishi Teddy Kilanga,Arusha 

Akizungumza na waandishi wa habari Desemba 9,2021,Mwenyekiti wa Bazecha jimbo la Arusha mjini,Emmanuel Zakaria amesema wanaomba maridhiano ya kitaifa ili haki itendeke kwa lengo la kuleta umoja wa vyama vya siasa nchini.

"Njia ya kuleta umoja ni kukaa meza moja katika kujadiliana kwa lengo la kupata muhafaka wa maridhiano kama ilivyo Zanzibar kwani hatuwezi tukafika hivyo inabidi tuige mfano wa Rais mstaafu Aman Abed Karume nakupata ujasiri aliyoutumia kuleta suluhu Tanzania visiwani,"amesema Mwenyekiti huyo.

Zakaria amesema sasa hivi Tanzania visiwani ipo amani katika vyama vya siasa kutokana na maridhiano yakukaa pamoja lakini kwa upande wa bara wamechoshwa na siasa za upande mmoja hivyo ni vyema wakakutana na Rais Samia kwa lengo la kuleta umoja na maendeleo nchini.

Mwenyekiti huyo amesema Rais Samia hana shida yeyote isipokuwa washauri kwani alipoingia madarakani alianza vizuri hadi wapinzani tulimuunga mkono hali iliyopelekea kukosa hoja kwa upande wao lakini wanashangaa kubadilika.

"Tunaomba Rais Samia arejee hotuba yake ya bungeni kwani sisi wazee wa jiji la Arusha tunaunga mkono maombi ya balozi wa Marekani aliyesema anatamani bara kuwe na maridhiano kama Zanzibar kwani najua hii ndio njia ya kuliponya Taifa hili,"amesema Zakaria.

Hata hivyo amemuomba Rais Samia katika hotuba zake ajikite  katika changamoto za wananchi wake kwani kunamifumuko ya bei ya vitu mbalimbali hali ambayo wenye maisha ya chini wanashindwa kukidhi.

Aidha amesema ni vyema wangewekeza zaidi katika rasilimali watu kwa kuanzia shuleni,wanafunzi wakapata chakula ambacho kinajumuisha mlo kamili ili kupata Taifa lenye nguvu katika kizazi cha sasa na kijacho.

Amesema kwa kufanya hivyo kutasaidia kupata Taifa lenye nguvu,wabunifu,hodari katika matumizi ya teknolojia pamoja na michezo.

Grace Liazer ambaye ni mjumbe wa baraza hilo amesema wanamuomba Rais Samia ajikite pia katika masuala ya bima kwa wananchi wote kwani wengi wao wanashindwa kumudu gharama za matibabu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI