Header Ads Widget

PROFESA MBARAWA SEKTA YA UJENZI NI KIGEZO CHA KUKUZA NA KUENDELEZA UCHUMI

 



Waziri  wa ujenzi na uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa sekta ya ujenzi kwa muda mrefu imekua kigezo cha kukuza na kuendeleza uchumi wa nchi kwani kuna uhusiano mkubwa wa uwekezaji na sekta ya ujenzi.....NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA


Mbarawa aliyasema hayo wakati akifungua kongamano la 31 la wahandisi (IET) lilifanyika mkoani Arusha ambapo alisema kuwa sekta hiyo ni muhimu na yakipekee  na  mifumo ya miundombinu ikiwa vizuri itarahisisha upatikanaji wa masoko na huduma nyingine katika kufikia maendeleo.



Aidha aliwataka waandishi kuwa wabunufu na wenye weledi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali kwani serikali  inawategemea wao katika kufikia mapinduzi ya kiuchumi na wana wajibu mkubwa katika seluala hilo hivyo watekeleze wajibu wao ipasavyo ili watanzania waweze kunufaika na miradi inayoendelea pamoja na inayotarajiwa kiwanza.


“Katika kazi zenu tumieni fursa kikamilifu kuingia katika ushindani ili kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu kwani uhandisi ni muhimili mkubwa unaowezesha kujua kwa sekta zote ambapo kwa mwaka 2020 hapa nchini kwani pamoja na sekata nyingine kuchangia pato la taifa ikiwemo kilimo na huduma nyingine zinazohusisha usafiri sekta hii kwa maana ya viwanda inachangia kwa asilimia kubwa,” Alisema Profesa Mbarawa. 




Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela Alisema kuwa wanajua ni nini umuhimu wa wahandisi katika maendeleo ya nchi kwani taaluma yao inalenga kuimarisha zaidi maendeleo ya nchi ambapo ni ukweli usiopingika kuwa wahandisi wamefanikisha miradi mbalimbali ambayo kwa Sasa ina manufaa makubwa kwa nchi.







Kwa upande wake Rais wa Tasisi ya wahandisi (IET) Injinia Sayed Rizwan Qadri alisema kuwa tasisi hiyo ina jumla ya wanachama 4568 lakini idadi hiyo ni ndogo kulingana na idadi ya wahandisi waliosajiliwa ambayo ni 32,145 hivyo wahandisi wajiunge katika tasisi hiyo kwani wingi wa wanachama ndio wingi wa mafanikio.


Alisema kuwa wanaishukuru serikali kwa kutambua ushiriki wahandisi katika kuchangia uchumi imara ambapo ni jukumu lao kufanya kazi kwa na mabadiliko ya teknolojia ili kuendana na kasi iliyopo kwa sasa katika ulimwengu.


“Ni wakati muafaka wa kuanza kuwatumia wanasayansi,wahandisi na mafundi wabobezi waliopo ndqni na nje ya nchi ili kuendana na kasi ya teknolojia na uchumi lakini pia natoa pongezi kwa serikali kwa utekelezaji wa miradi yote mikubwa kwa kiwango cha mataifa,” Alisema Injinia.




Pia mkutano huo umeenda sambamba na uwekaji sain hati ya makubaliano kati ya tasisi ya wahandisi Tanzania na Tasisi ya wahandisi washauri Tanzania ambapo wote kwa pamoja wameona umuhimu wa kushirikiana kama jamii moja na kuwa na nguvu ya pamoja katika kutatua changamoto na kuendeleza maendeleo ya nchi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI