Header Ads Widget

RAIS SAMIA KUFUNGUA KIWANDA CHA KUTENGENEZA NYAYA ZA MKONGO WA MAWASILIANO KESHO

 



KATIKA kuelekea miaka 60 ya uhuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kesho atazindua kiwanda cha kutengeneza nyaya za mkongo wa mawasiliano cha Raddy Fibre Manufacturing (T) Ltd kilichopo wilaya ya Mkuranga.


Aidha kiwanda hicho ni kikubwa cha nne Barani Afrika cha kutengenezea nyaya zinazotumika kutengeneza mkongo wa mawasiliano.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mjini Kibaha Abubakari Kunenge alisema kuwa kiwanda hicho ni moja ya viwanda vikubwa Afrika baada ya vile vya Misri, Algeria na Afrika ya Kusini vinavyotengeneza teknolojia hiyo.


Kunenge alisema kuwa kiwanda hicho kitatoa huduma kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati ambapo Tanzania inaendelea kupiga hatua kwenye uwekezaji mkubwa.


"Tunamshukuru Rais kwa kutupa heshima ya kuja kwetu kuzindua kiwanda hicho ikiwa ni sehemu ya kuelekea miaka 60 ya Uhuru," alisema Kunenge.


Alisema kuwa mbali ya kutembelea kiwanda hicho atasimama eneo la Vikindu na kuzungumza na wananchi.


"Atazungumza na wananchi, viongozi wa kisiasa, wazee maarufu, viongozi wa dini na watu mbalimbali,"alisema Kunenge.


Aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili kumsikiliza ujumbe atakaowapa juu ya masuala mbalimbali ya maendeleo.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI