Header Ads Widget

NYUMBA 133 ZA KIJIJI CHA LIKUYUSEKAMAGANGA ZA EZULIWA NA MVUA ILIYOAMBATANA NA UPEPO MKALI.

 

 


  



NYUMBA 133 za Kijiji cha Likuyusekamaganga Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma zimeezuliwa na mvua iliyoambana na upepo mkali na kusababisha kaya hizo kushindwa mahali pakuishi.



 Akizungumzia tukio hilo mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Dr.Julius Ningu amesema kuwa tukio hilo  lililodumu kwa dk 45 hivi limetokea Novemba 30 mwaka huu majira ya saa 10:30 jioni ambalo pia limesababisha majeruhi nane ambao saba wametibwa na kuruhusiwa huku mmoja akiwa bado katika hospitali ya Wilaya ya Namtumbo.




  Dr.Ningu amesema kuwa licha ya kuezuliwa kwa nyumba hizo bado kumeezuliwa madarasa matatu na ofisi ya walimu ya  shule ya Msingi ya Likuyusekamaganga pamoja na Zahanati.



 Amesema kuwa kufuatia maafa hayo Serikali imepeleka watalaam wa kutadhimini uharibifu wote ambao umejitokeza ili Serikali iweze kufanya haraka namna ya kulejesha miundombinu ya shule pamoja na Zahanati hiyo .




Kwa upande wake diwani wa kata ya Likuyuseka Kassim Gunda amesema kuwa mvua hiyo imesababisha maafa makubwa na kuwa wananchi ambao hawajapatwa na maafa hayo wameombwa wasaidiane na wananchi ambao wamepatwa na majanga katika sehemu za kujihifadhi wakati serikali ikiendelea na taratibu zingine.



 Naye Mwalimu wa Shule hiyo Joachimu Komba amesema kuwa uharibifu huo hasa wa madarasa utaadhili kama endapo hatua za haraka hazitafanyika kwa kuwa Januari 2022 wanafunzi wapya wanatakiwa kusajiliwa .


                


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI