Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela amekabidhiwa na kuzindua vyumba 9 vya madarasa katika shule 5 za sekondari halmashauri ya Arusha, huku akiwapongeza wasimamizi wa mradi huo kuanzia ngazi ya wilaya, halmashauri, kata, viongozi wawakilishi wa wananchi pamoja na wananchi wote kwa ushiriki wao, kwa kukamilisha miradi hiyo kwa viwango na kwa wakati.........NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Mongela alitoa pongezi hizo mara baada ya kuridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa ya Mpango wa Maendeleo ya Ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19, ambapo alipokea na kuzindua madarasa 9, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi hiyo katika halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru.
“Ninawapongeza wananchi wote wa halmashauri ya Arusha kwa ushirikiano mliuonesha katika kutekeleza mradi huu wa ujenzi wa madarasa, madarasa yamejengwa kwa viwango vinavyohitajika na kukamilika kwa wakati, madarasa yanavutia, hii maomesha dhahiri namna gani mnaunga mkono agenda ya mheshimiwa Rais, mama Samia ya kuboresha huduma za jamii na kuondoa kero kwa wananchi, hongereni sana ofisi ya mkuu wa wilaya, timu ya watalamu halmashauri, waheshimiwa madiwani pamoja na wananchi wote kwa ujumla wenu,” alisisitiza Mongela
Aidha aliwataka wananchi kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2022, wanaanza masomo kwa wakati, na kuwataka kuendelea kushiriki utekelezaji wa miradi yote inayotekelezwa katika maeneo yao, kwa kuwa serikali imeleta fedha nyingi katika miradi ya elimu, afya, maji na barabara, serikali inahitaji ushiriki wa wananchi, ushiri ambao utawezesha umiliki wa wananchi wa miradi hiyo baada ya kukamilika.
Pia aliwaagiza watendaji, wanachi na wadau wa maendeleo wa halmashauri hiyo, kuweka mkakati wa kukamilisha miradi mingine ya madarasa ambayo imejengwa kwa nguvu za wanachi na haijakamilika katika shule za halmashauri hiyo na kuhakikisha, miradi hiyo inakamilika ili wanafunzi watumie madarasa hayo.
Katika ziara hiyo viongozi wawakilishi wa wananchi, wameipongeza na kuishukuru serikali ya awamu ya sita na juhudu za mhesimiwa Rais, mama Samia Suluhu kwa kuelekeza fedha nyingi, kiasi cha shilingi bilioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za halamshauri ya Arusha, jambo ambalo wamekiri halijawahi kutokae na kuongeza kuwa, fedha hizo za ujenzi wa madarasa zimekuja wakati muafaka kwa kuwa kila mwaka, wananchi hulazimika kuchangishana kujenga madarasa ya kidato cha kwanza kwa mwaka unaofuata.
Diwani wa kata ya Bangata Mhe. Ezra Tomito alisema kuwa licha ya kuwa madarsa hayo yatawanufaisha watoto wao, lakini kwa kiasi kikubwa yamewapunguzia wananchi mzigo wa kuchangishana fedha za ujenzi wa madarasa, zoezi ambalo hufanyika kila mwaka nyakati kama hizo.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango, alimshukuru mkuu wa mkoa wa Arusha, kwa kukuabali kupokea na kuzindua vyumba 9 vya madarasa, kama mfano wa madarasa yote yaliyokamilika katika halmashauri ya Arusha, na kumuhakiksihai kuendelelea kusimamia utekelezaji wa majukumu ya serikali ya kuwatumikia wananchi, pamoja na kuyafanyia kazi maagizo yote aliyoyatoa ikiwemo kusimamia fedha zilizoletwa kwa ajili ya kutekeleza miradi katika sekta zote na kuweka mkakati wa kukamilisha miradi viporo ya madarasa katika shule.
Katika ziara hiyo, Mkuu wa mkoa wa Arusha, ametembelea jumla ya miradi 8 yenye thamani ya shilingi milioni 860, miradi 7 ya sekta ya elimu na mradi mmoja wa upanuzi wa kituo cha Afya Oldonyosmabu unaogharimu shilingi milioni 200.
0 Comments