Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi amekabidhi msada vifaa mbalimbali vya ujenzi kwa Chama ushirika wa akiba na mikopo Cha umoja saccos iliyopo kata ya Kimochi wilaya Ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
Akikabidhi vifaa hivyo mbunge huyo amesema kuwa amemua kutoa msaada huo kutokana na urafiki uliyopo kati yake na wao ambapo pia ameipongeza saccos hiyo kwa kusimama na kuendeza miradi ya maendeleo Kama ujenzi wa Ofisi Yao wenyewe.
Aidha amesema kuwa ameweza kukabidhi jumla ya mifuko 50 ya saruji, lori mbili za mchanga na fedha za ufundi katika chama cha Ushirika cha akiba na mikopo , vyote vikiwa na thamani ya Shilingi Milioni 1.4.
Amesema kuwa hiyo ni tasisi muhimu kwa watu ambao hawataweza kupata huduma kwenye zile taasisi kubwa za kibenki.
Meneja wa chama hicho Kulwa Mgeni amemshukuru mbunge huyo kwa msaada alioutoa wa vifaa vya ujenzi wa Ofisi ya umoja saccos limited.
Amesema kumalizika kwa ujenzi wa jengo hilo kutarahisisha huduma za kibenki pamoja na zile za chama kwa Wanachama na wananchi wa eneo hilo.
Naye diwani wa Kata hiyo ya Kimochi Ally Badi amesema ni hatua muhimu inayopaswa kuungwa mkono ili kufikisha huduma za kifedha karibu na wananchi.
0 Comments