Baraza Kuu la waislamu Tanzania ( BAKWATA) mkoa wa Kilimanjaro limeazima kufanya miradi ambayo itawasaidia waumini wa dini ya kiislamu kutokana na shida, matatizo na dhiki ambayo imewakumba waislamu katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Miradi hiyo ni miradi ambayo italeta Chachu ya maendeleo lakini lengo kuu ni kusaidia watoto yatima ,wajane,watu wasiojiweza ,kuongeza idadi ya misikiti na vitu vingine ambavyo uislamu unakabiliwa ili kuweza kuvitatua.
akizungumza na wandishi wa habari mkoani Kilimanjaro Shekhe wa mkoa wa Kilimanjaro amesema kuwa wamejipanga katika hilo na kuwataka makatibu wote wa wilaya na misikiti kubuni miradi mipya ambayo itakuwa chanzo Cha kujiinua kiuchumi.
Katika hatua nyingine amesema kuwa baraza la waislamu Tanzania (BAKWATA) mkoa wa Kilimanjaro imeandaaa sherehe za maulid ya kumuadhimisha mtume Muhammad swalala waley wasalam ambayo itafanyika tarehe 15 January mkoani. hapa.
Mlewa amesema kuwa katika maulidi hayo yataambatana uzinduzi wa ramani ya msikiti wa mkoa utakaojengwa katika maeneo ya Bakwata.
Aidha amewaomba viongozi wa ngazi zote za mkoa ,wilaya,kata mpaka misikiti ,Kama ilivyokuwa zama za nyuma kuhudhuria sherehe hizo za maulid zinazotarajia kufanyika .
0 Comments