Katika kukuza Sekta ya ajira nchini Tanzania,Kampuni ya Global light imekuja na mfumo rafiki wa ukataji tiketi ambao utasaidia kurahisisha kwa wateja kupata usafiri kwa wakati pamoja na kutoa fursa kwa wakala....Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam
Akizungumza na waandishi wa habari mapema Leo hii Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ambae pia ni mwendeshaji wa mfumo huo, Raymond Magambo amesema kuwa, mfumo huo unakwenda kumaliza tatizo la abiria kusumbuka wakati wa usafiri wanapohitaji tiketi za mabasi.
"Kumekua na changamoto nyingi ambazo wamekua wakikutana nazo pindi wanapotaka kusafiri, kupitia mfumo huu itasaidia abiria kusafiri kwa wakati na salama kwani mfumo huu umelenga kumaliza changamoto za wasafiri"amesema Magambo.
Aidha amesema kuwa,mfumo huo umeunganishwa na Mamlaka ya mapatoa (TRA), Taasisi za kifedha, mitandao ya simu Airtel money, Mpesa,Tigo pesa na Mabenki yote ikiwemo NMB, CRDB,NBC, na wamiliki wa gari ambapo kupitia mfumo taondoa usumbufu na upotevu wa fedha.
Aidha, amesema mfumo huo pia umezingatia watu wa kawaida ambao hawatumii simu janja wataweza kukata tiketi zao bila usumbufu na kupata tiketi, hivyo ni amewaomba watanzania wote kutumia mfumo huo.
Ameongeza kuwa, mfumo huo pia utatumika nje ya nchi, ambapo utaanzia Tanzania ambapo umefikisha miaka sita tangu kuanzishwa kwake.
Kwa upande wake, Mkurugenzi idara ya ufundi Global light, James Chambo amesema mashine ziko tayari kuanza kutumika na mawakala wataanza kuhudumia wateja bila kujali umbali waliopo huku wakihakikisha Serikali inapata kodi yake na mmiliki wa basi anapata fedha yake
Naye Mwenyekiti wa mawakala wa mabasi ya Mkoa Dar es salaam, Hamisi Iddy mfumo huo unatakiwa kutangazwa pia katika Stendi ya Magufuli iliyoko mbezi mfumo huo ili wale wote wanaokata tiketi mkononi waepukane ma usumbufu ambao wamekua wakiupitia wa kupata usafiri.
Naye Mwenyekiti wa chama cha kutetea abiria. (CHAKUA) Modest Nkurlu amesema hivi karibuni akiwa katika utekelezaji wa majukumu yake alikutana na abiria 26 waliokaa kuanzia asubuhi mpaka jioni kwa kukosa usafiri hivyo ni vyema kabla mtu hajaanza safari Bora akiwa nyumba akate tiketi kwa wakala au kwa njia ya mtandao asiwategemee wakata tiketi mkononi pale stendi.
0 Comments