Askari wa jeshi la akiba (MGAMBO) wametakiwa kuyatumia mafunzo hayo kuilinda nchi yao kwani nchi hujengwa na kila mwananchi na sio kwenda kufanyia vitendo vya uhalifu
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Ngolo Malenya wakati akifunga mafunzo ya Jeshi la akiba Wilayani Ulanga Mkoani Morogoro katika viwanja vya mapinduzi,na kusema kuwa ulinzi wa Nchi ni wa kila Mtanzania hivyo hao vijana waliohitimu mafunzo hayo wanatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha nchi inakuwa salama
Ngolo amesema kuwa mafunzo waliyopata yatawasaidia kupata kazi sehemu mbalimbali ikiwemo kwenye taasisi mbalimbali na makampuni ya ulinzi hivyo amewataka vijana hao kuwa na subira kwa kuwa sasa wanafahamika baada ya kuhitimu mafunzo yao
Naye Mshauri wa Mgambo Wilayani Ulanga Meja Kevin Byabato amesema kuwa wakati wanaanza mafunzo kulikuwa na jumla ya wanafunzi 80,lakini mpaka wanamaliza kulikuwa na jumla ya wahitimu 77 ambapo watatu walishindwa kumaliza mafunzo hayo na kuishia njiani
Aidha Meja Byabato amesema kuwa wanatoa mafunzo hayo kwa lengo la kusaidia vijana kuijenga Nchi yao hivyo yeyote atakaye kwenda kinyume na sheria za Nchi hatua kali itachukuliwa dhidi yake na Jeshi halitahusika kumtetea.
0 Comments