Header Ads Widget

DC ULANGA ATAKA WATU KUPIMA VVU



Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Ngolo Malenya amewataka wananchi wote Wilayani hapa kuwa na desturi ya kujitokeza mara kwa mara kupima VIRUS vya UKIMWI  ili kujitambua kama wameambukizwa kuanza kutumia dawa kabla hawaadhirika.



Akizungumza na wananchi pamoja na viongozi mbalimbali waliojitokeza katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani wilayani ulanga,Malenya amesema kuwa ugonjwa wa UKIMWI upo na unendelea kuwa tishio kwa wananchi, hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini katika kujilinda na kutambua afya zao mara kwa mara.



Malenya amesema kuwa maambukizi kwa Wilaya ya Ulanga yameongezeka kutoka asilimia 3.7 mpaka kufikia asilimia 4.2 hivyo wananchi wanatakiwa kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha wanapambana na ugonjwa huo ambapo kila mwananchi achukue hatua ya kupima kila  baada ya miezi mitatu


 

Aidha mkuu huyo wa Wilaya amewataka wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kupata chanjo ya ugonjwa uvico 19 kwani chanjo hiyo inatolewa bure wilayani Ulanga kwa wananchi wote wanaotaka kupata chanjo hiyo.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI