Header Ads Widget

CHEMCHEM CUP 2021 RASMI KUTIMUA VUMBI BABATI


Mkuu wa wilaya ya Batati Lazaro Twange akisalimia na wachezaji wakati wa ufunguzi wa michuano ya kombe la CHEMCHEM 2021

Michuano ya chemchem CUP yenye lengo la kupambana na ujangili, katika eneo la hifadhi ya jamii ya wanyamapori ya burunge,imezinduliwa jana na Mkuu wa wilaya ya Babati mkoani Manyara,Lazaro Twange.

Michuano hiyo, inashirikisha timu 10 ambazo zinatoka katika vijiji ambavyo vinaunda jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori ya burunge.

Akizindua michuano hiyo, Twange aliwataka wachezaji kuitumia vyema kukuza vipaji vyao lakini pia kupambana na ujangili na kutunza mazingira.

Meneja wa miradi wa taasisi ya chemchem fondation ambao ndio wadhamini wa ligi hiyo, Peter  Millanga alisema leo la wao kuandaa michuano hiyo ni kuwashirikisha vijana katika uhifadhi.

Alisema  wachezaji ambao wanashiriki pia wanapata fursa za kukuza vipaji vyao kwani tayari kuna wachezaji wametoka katika ligi hiyo na kuchezea ligi kuu.

“tunataka michuano hii kutumika katika kuhamamisha uhifadhi, kupiga vita ujangili lakini pia wachezaji kutunza mazingira”alisema

Mratibu  wa michuano huyo, Bura Bayo alizitaja timu ambazo zitashiriki ni Olasiti FC, Minjingu FC,Mdori Fc,Mshikemshike FC,Macedonia FC, Youngboys,Macklion FC, Star Boys,Gembwe na Sangaiwe .

Alisema kiasi cha sh 2 milioni kitatolewa kama zawadi katika michuano hiyo ambayo inatarajiwa kumalizika Desemba 29.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI