Header Ads Widget

BARAZA LA VYAMA SIASA LAZITAKA JUMUIYA ZA KITAIFA KUTOWAINGILIA, VIONGOZI WA VYAMA WATAKIWA KUSHIRIKI MKUTANO

 



Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa nchini Tanzania Juma Ali Khatib amezitaka jumuiya za kimataifa kushirikiana nao katika kudumisha uhuru na amani, hivyo, isitokee Taasisi au mtu yoyote kiwapangia cha kufanya........Na Fatma Ally MDTV Dar es salaam


Aidha, amevitaka vyama vya siasa nchini  Tanzania vilivosajiliwa kushiriki katika Mkutano utakafanyika Dec 16 na17 mwaka huu  jijini Dodoma ambao umelenga kujadili mambo mbalimbali ikiwemo  sheria,demokrasia pamoja na maadili ya kitaifa.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema leo hii, kuelekea kilele cha maadhimisho siku ya uhuru ambapo amesema kuwa, ni muhimu vyama vyote kuweza kushiriki katika Mkutano huo ambao utafinguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.


"Tanzania ni nchi ya kuigwa duniani tumekua na vitu vya kujivunia ikiwepo amani, uhuru pamoja na kuendesha Umoja wa kitaifa tumefanikiwa sana, hivyo, tunaomba watu wasituimgilie wasipangie cha kufanya."amesema Khatib.


Hata hivyo, baraza hilo limeishukuru Serikali chini ya Rais Samia kwa kukifanya chombo hicho kuwa cha sheria, hivyo ameahidi kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha vyama vya siasa vinakua na umoja na mshikamano..


Kwa upande wake, John  Cheyo ambae ni  Mwenyekiti kamati ya fedha ya Baraza la vyama vya siasa, amewataka vijana na watanzania kwa ujumla wamlaani yoyote anaetaka kuidhihaki nchi ya Tanzania.


"Nawaomba sana watanzania tuipende nchi yetu, hatuna nchi nyengine ya kwenda asitokee kiongozi yoyote kutoka nje ya nchi au kiongozi wa vyama vya siasa kuweza kufanya dhahaka "amesema Cheyo.


Aidha, ameimba Serikali kudumisha uhuru na amani uliopo, kupitia baraza hilo, hivyo amewataka viongozi wa vyama vya siasa kua na Umoja na mshikamano .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI