Mabaraza haya hupokea masuala ya madai, jinai na kuangalia migogoro ya ardhi. Rufaa zake zote za mashauri yanayo husiana na ardhi hupelekwa kwenye Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya.
Muundo wa Baraza la Kata; Ni chombo cha utatuzi wa mashauri mbalimbali katika ngazi ya Kata kinachoundwa na wajumbe 4 hadi 8 ambapo kati yao wanawake watakuwa 3. Wajumbe wa Baraza huteuliwa na Kamati ya Maendeleo ya Kata. Baraza la Kata linaundwa na Sheria ya Mabaraza ya Kata Namba 7 mwaka 1985.
Hata hivyo katika utatuzi wa migogoro ya ardhi Baraza huongozwa na Sheria ya Mabaraza na Mahakama za Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi Namba 2 ya mwaka 2002. Sifa za wajumbe wa Baraza la Kata. Huwa awe mtu yeyote mkazi wa vijiji vinavyounda kata husika, Kwanza awe raia wa Tanzania, aliyetimiza miaka 18 na mwenye akili timamu. Asiwe mbunge, Diwani, mjumbe wa Halmashauri ya Kijiji, Baraza la Ardhi la Kijiji,
Pia, Asiwe mjumbe wa Halmashauri ya Kijiji au Kamati ya Maendeleo ya Kata, Asiwe mwanasheria au mtu yeyote aliyeajiriwa katika idara ya mahakama. Asiwe mtu aliyewahi kutiwa hatiani kwa kosa la jinai ama utovu wa kukosa uaminifu. iii. Kipindi cha ujumbe na Majukumu ya Baraza la Kata Kila mjumbe atatumikia Baraza kwa kipindi cha miaka 3 tokea tarehe ya kuchaguliwa kwake na kila mjumbe anaweza kuteuliwa tena kwa kuzingatia taratibu zile zile za awali.
Jukumu la msingi la Baraza ni kuleta amani, utulivu na mapatano katika eneo lake kwa mujibu wa Sheria za Ardhi za mwaka 1999 na Sheria ya Mabaraza na Mahakama za Ardhi ya mwaka 2002. Uongozi wa Baraza la Kata Baraza litaongozwa na Mwenyekiti atakayeteuliwa na Kamati ya Maendeleo ya Kata miongoni mwa wajumbe wa Baraza la Kata waliochaguliwa. Katibu wa Baraza la Kata atateuliwa na Halmashauri ya Wilaya ambamo Baraza hilo limo baada ya kupata uthibitisho wa Kamati ya Maendeleo ya Kata.
Katibu wa Baraza anaruhusiwa kutumikia baraza kwa muda wa miaka Mitano (5) na anaweza kuteuliwa kwa awamu nyingine. Vikao vya Baraza la Kata a. Katika vikao vya usuluhishi vya Baraza lazima liwe na wajumbe 3 na angalau mmoja awe mwanamke. Baraza litaweka kumbukumbu za vikao vyote. Baraza litatakiwa kujitahidi kupata suluhu na linaweza kuahirisha kesi endapo litafikiria kuwa kufanya hivyo suluhu inaweza kupatikana. Mambo ya kuzingatia wakati wa Suluhu. Kuzingatia mila na desturi. Kuzingatia haki za asili za watu. Kuzingatia njia mbadala za utatuzi
Baraza lina ukomo wa aina mbili katika kufanya kazi zake: Ukomo wa kieneo. Baraza lina uwezo wa kushughulikia migogoro ya mali au ardhi iliyopo ndani ya kata inayohusika. Ukomo wa kifedha. Baraza lina uwezo wa kusikiliza na kutoa maamuzi juu ya mgogoro wowote ambao mali au ardhi inayogombaniwa thamani yake haizidi shilingi milioni tatu (3,000,000).
Uwezo wa kimamlaka wa Baraza la Kata Baraza linaweza kutoa amri za kimahakama kama zifuatazo: Kuagiza urejeshwaji wa ardhi iliyonyang’anywa. Kumtaka mtu atimize wajibu wake ndani ya mkataba. Kutoa amri au maagizo ya kisheria. Kuagiza ulipaji wa gharama zitakazokuwa zimetumiwa na atakayeshinda kesi au mashahidi wake. Kutoa agizo lolote ambalo litakuwa la haki kwa uamuzi utakaotolewa.
Ukataji Rufaa kutoka Baraza la Kata Upande wowote ambao hautaridhika na maamuzi ya Baraza la Kata unaweza kukata rufaa katika Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ndani ya siku 45 tangu siku ya kutolewa uamuzi.
makwadeladius@gmail.com
0717649257.
2 Comments
Malala nzuri.....tunaomba sampo ya kiapo cha wajumbe wa Baraza la ardhi la kata.
ReplyDeleteNaomba kujua utaratibugani hutumika kwa mkata RUFAA aliyechelewa mda wa rufaa take.
ReplyDelete