Header Ads Widget

ANYONYESHA MAPACHA WANNE BAADA YA MAMA YAO KUFARIKI ,AOMBA MSAADA

 


Salma Abdalah (28) mkazi wa mtaa wa Mfuruni kata ya Tungi Manispaa ya Morogoro analazimika kunyonyesha mapacha wanne baada ya mdogo wake  latifa Abdal( 26) kujifungua mapacha wawili na kufariki huku nae akijifungua mapacha wawili jambo ambalo linamlazimu kunyonyesha watoto wote wanne.


Kituo huki kimefika nyumbani anapoishi mama huyu ambapo anasema kuwa baada ya mdogo wake kujifungua mapacha wawili alianza kusumbuliwa na tumbo na wiki moja baadae akafariki hivyo kutokana na hali ya maisha kuwa ngumu analazimika kunyonyesha watoto wa mdogo wake kutokana na kukosa fedha za kuwanunulia maziwa kila siku .


Salma anasema wakati mdogo wake anafariki ameacha jumla ya watoto watano huku nae akiwa na watoto sita jambo ambalo kwa sasa analazimika kulea familia ya watoto kumi na moja ambapo ameomba msaada wasamalia wema kumsaidia kupitia namba 0789695698


 Iddi Malilo ni daktari bingwa wa watoto anatolea ufafanuzi  suala la watoto wa mama mwingine kunyonya maziwa na mama mwingine ambapo amesema kuwa hakuna madhara ya kiafya endapo kati ya mama na mtoto  hawana magonjwa ya virusi au batkeria.


MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS