Header Ads Widget

ZAHANATI FUKAYOSI YAPATA VIFAA TIBA

Zahanati ya kata ya Fukayosi wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani imepokea msaada wa vifaa tiba wenye thamani ya shilingi millioni tano kutoka kwa kanisa la Penuel lililopo katika kata hiyo ili kusaidia kupunguza changamoto ya vifaa tiba katika zahanati hyo.

Akikabidhi msaada huo kwa mganga wa zahanati ya Fukayosi afisa tarafa ya Yombo Gladness Shafii alimpongeza mwenyekiti wa kitongoji Cha fukayosi Rajabu Mkeche- ambaye amefanikisha upatikani wa vifaa hivyo na kuwaomba viongozi wengine kuiga mfano huo katika maeneo yao ili kusaidia kutatua changamoto mbalimbali zilizopo.

"Jambo hili sio dogo alichofanya mwenyekiti wa kitongoji  Mkecha ni jambo la kuigwa kusaidia kupunguza changamoto ya uhaba wa vifaa tiba na viongozi wengine naomba muige mfano huu."alisema Shafii'

Pia mwenyekiti wa chama Cha mapinduzi kata ya Fukayosi Olenjale Machanje alisema kuwa juhudi zinazooneshwa na mwenyekiti wa kitongoji ni kubwa ameonesha njia kwa utendaji kazi wake kwa namna alivyoboresha barabara za mitaa, na hili suala ya vifaa tiba katika zahanati na kuwasihi wengine kuiga juhudi hizo na sio kukatishana tamaa.

"Jambo hilo ni kubwa sana kitongoji kutafuta mbinu za kuwasaidia wananchi ndio uongozi na sio kukatishana tamaa kwa kusemeana maneno ya kurudishana nyuma nawaomba sana kuonesha ushirikiano na kuleta maendeleo kwa wananchi."Alisema Machanje.

Rajabu Mkecha ambaye ni mwenyekiti wa kitongoji Cha fukayosi aliyefanikisha upatikani wa vifaa hivyo alisema kuwa kiongozi ni kuonesha njia ili wananchi wasione aliyekuwapo ni mwema zaidi ya aliyepo hivyo atahakikisha wanaendelea kuleta mabadiliko katika sekta mbalimbali ili kuleta maendeleo kwa wananchi.

"Wananchi wa fukayosi nafasi hii niliyonayo ni kubwa nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kutafuta wadau mbalimbali kushirikiana na kitongoji na kwa sasa tunatarajia kupata msaada mwingine wa kujengewa vyumba vya madarasa na kuletewa komputa katika shule ya msingi."Alisema Mkecha.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI