Header Ads Widget

KATIBU MKUU JUMUIYA YA MADOLA AKUTANA NA WAZIRI JAFO, GLASGOW SCOTLAND

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Selemani Jafo akimsikiliza Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Patricia Scotland katika moja ya mikutano inayoendelea Glasgow Scotland. Jumuiya hiyo imeonyesha nia ya kuisaidia Tanzania katika jitihada za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Kikao hicho kimefanyika leo Novemba 10, 2021 Glasgow Scotand.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Patricia Scotland akimkabidhi nyaraka mbalimbali kutoka Jumuiya ya Madola mara baada ya Waziri Jafo kumtembela katika Ofisi yake Glasgow, katika Mkutano wa Mabadiliko ya tabianchi unaoendelea nchini Scotland.

Katibu Mkuu wa jumuiya ya Madola Bi. Patricia Scotland (kulia) akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) alipomtembelea katika ofisi za Sekretarieti za jumuiya hiyo. Kushoto ni Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI