WAZIRI SIMBACHAWENE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA KUSIMAMIA, KUDHIBITI NA KURATIBU MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YAKE, JIJINI DODOMA, LEO
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia, Kudhibiti na Kuratibu Mapato na Matumizi ya Wizara, George Simbachawene, akizungumza katika kikao cha kupitia taarifa ya Kamati hiyo kwa Robo ya Kwanza ya Mwaka wa Fedha 2021/2022, kilichofanyika jijini Dodoma, leo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Wajumbe wa Kamati ya Kusimamia, Kudhibiti na Kuratibu Mapato na Matumizi ya Wizara wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (hayupo pichani), wakati alipokuwa akizungumza katika kikao cha kupitia taarifa ya Kamati hiyo
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia, Kudhibiti na Kuratibu Mapato na Matumizi ya Wizara, George Simbachawene (kushoto), akisalimiana na Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mbaraka Semwanza, wakati alipokuwa anawasili katika kikao
0 Comments