Header Ads Widget

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAFANIKIWA KUTEGUA MITEGO 380 YA KUULIA WANYAMAPORI KATIKA HIFADHI YA NYERERE


Wizara ya Maliasili na Utalii  imefanikiwa kutegua nyaya za umeme 380 zilizokuwa zimetegwa katika Hifadhi ya Taifa ya Nyerere ikiwa ni aina mpya ya ujangili wa wanyamapori kwa ajili ya kitoweo

 Akizungumza  hivi karibuni, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro  akiwa ameambatana na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania,  Regine Hess  katika Hifadhi ya Taifa ya Nyerere iliyopo mkoani Morogoro ameishukuru Serikali ya Ujerumani kwa kufadhili mradi huo wa kunasua mitego iliyotegwa kwa ajili ya kuuwa wanyamapori katika Hifadhi hiyo

Alisema  Majangili  hao wamekuja na mbinu mpya mara baada ya Serikali kupambana na ujangili wa Biashara ya wanyamapori wakubwa kama vile tembo pamoja na faru

Dkt. Damas Ndumbaro alisema ujangili wa wanyamapori kwa ajili ya kitoweo kwa kutumia nyaya za umeme umeanza kuchukua sura mpya   huku Serikali ikiahidi kuendelea kupambana na mbinu  hiyo mpya

Dkt. Ndumbaro alisema tokea kikosi maalumu kilichoundwa kwa kushirikiana na wanavijiji kwa ajili ya kutegua mitego hiyo jumla ya wanyamapori watatu walikutwa wamekufa mara baada ya kunaswa kwenye mitego hiyo

Aliwataja wanyamapori hao waliokutwa wamekufa kuwa ni twiga mmoja pamoja na swala wawili hata hivyo Dkt. Ndumbaro alisema kupitia mradi huo wa kunasua mitego Wizara hiyo imekuja na mbinu ya kuwashirikisha wanavijiji wanaopakana na Hifadhi kwa ajili kupambana na majangili hao.

Akizungumzia aina mpya hiyo ya ujangili, Dkt. Ndumbaro alisema majangili hao wamekuwa wakitega mitego hiyo kwa ajili ya kuwanasa wanyapori ili kujipatia nyama ya kula.

Dkt. Ndumbaro alisema licha ya mitego hiyo kutegwa ajili ya kuuwa wanyamapori wadogo wadogo kwa ajili ya kitoweo lakini mitego hiyo inaweza kunasa hata wanyamapori wakubwa kama vile tembo na wanyamapori wengine wakubwa 

Alifafanua kuwa baadhi ya Jamii  zimekuwa zikiendeleza imani potofu ya kula nyamapori kwa kuamini kuwa ndo nyama bora kupita zote kuwa  hali imekuwa ikichangia ujangili kwa ajili ya kitoweo.

Kwa upande wake Balozi wa Marekani nchini Regine Hess alisema Serikali yake iliamua kufadhili mradi wa kutegua mitego hiyo baada ya Serikali ya Tanzania kufanikisha kukomesha ujangili kwa asilimia 90 hususani ujangili wa biashara.

Hess alielezea kuwa mradi huo pia umeonesha mafanikio makubwa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambapo mitego mingi imeweza kuteguliwa.

Aidha, Balozi huyo aliipongeza Serikali ya Tanzania kuwa Serikali ya kwanza Barani Afrika kwa  kusimamia shughuli za uhifadhi kiukamilifu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI