Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Ludovick Nduhiye amesema kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii itatenga fedha ili kuhakikisha kuwa majengo ya taasisi zake yanafanyiwa ukarabati ikiwa ni pamoja na chuo Cha viwanda vya misitu Moshi kwa kuhakikisha kuwa majengo chakavu ya chuo hicho yanafanyiwa ukarabati ili kuboresha mazingira ya kujifunzia na kifundishia chuoni hapo.....Na Rehema Abraham
Nduhiye amesema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 24 ya chuo hicho ambapo amesema kuwa ni azma ya Wizara kuhakikisha kuwa majengo ya taasisi zake yanaendelea kuwa Bora bila kuhatarisha usalama wa wanafunzi na watumishi.
"Kwa takribani mwaka mmoja Sasa tangu nilipochaguliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara nimekuwa nilifanya kazi kwa kushirikiana kwa Ushirikiano wa karibu na uongozi wa chuo hiki ,na naahidi kutoa Ushirikiano kadri utakavyohitajika "Alisema Nduhiye.
Ameendelea kusema kuwa Atashirikiana na na viongozi wengine wa Wizara kuhakikisha suala la upatikanaji wa fedha za kutosha za ruzuku na miradi ya maendeleo kwa ajili ya chuo hicho linapewa kipaumbele.
"Mimi binafsi na Wizara kwa ujumla tutaendelea kushirikiana na mkurugenzi wa idara ya misitu na nyuki kuhakikisha kwamba,kiasi Cha fedha za ruzuku na Cha kugharamia miradi ya maendeleo zinapatikana kwa wakati"Alisema Nduhiye.
Awali akisoma taarifa fupi Kaimu mwenyekiti wa bodi ya ushauri wa chuo hicho Dokta Consolata Kapinga amesema kuwa chuo hicho kwa mwaka 2021 kimetoa wahitimu 216, ambapo wanaume ni 133, na wanawake ni 83.
Aidha ameongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2020/ 2021 Serikali imeajiri watumishi wapya katika chuo hicho hivyo kupungua kwa changamoto za uhaba wa watumishi.





0 Comments